Dawa ya kusugulia meno ni kemikali inayotumika pamoja na mswaki wa kisasa kusafishia meno yazidi kupendeza na kuwa na afya.

Dawa ya meno ikikamuliwa kutoka tyubu yake na kuwekwa juu ya mswaki wa kisasa ili kusambazwa katika meno yote.

Inasaidia kuondoa harufu mbaya, utambo wa meno na mabaki ya chakula katikati yake, pamoja na kuacha aina ya kinga (hasa ya floridi, kwa Kiingereza "Flouride") dhidi ya maradhi ya meno na ya ufizi (nyama inayoambatana nayo) (kwa Kiingereza "gingivitis").[1]

Hata hivyo kwa kiasi kikubwa ufanisi wa usafi unategemea zaidi matumizi ya mswaki wenyewe kuliko ya dawa hiyo.

Badala ya dawa ya meno vinaweza kutumika chumvi na magadi.

Dawa ya meno hayatakiwi kumezwa kutokana na floridi iliyomo. Ikimezwa kidogo si hatari sana, lakini kama ni kiasi kikubwa ni lazima kuomba msaada wa daktari.[2]

Dawa ya meno iliyotengenezwa kwa kusaga mifupa au chaza ilianza kutumika katika Ugiriki wa Kale na Roma ya Kale.[3]

Matumizi yake yalienezwa hasa katika karne ya 19.

Nchi mbalimbali zimekataza aina kadhaa za dawa ya meno kutoka China kwa sababu zina sumu aina ya diethylene glycol (kifupi diglycol au DEG).[4]

Tanbihi hariri

  1. American Dental Association Description of Toothpaste"Toothpaste". April 15, 2010. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-05. Iliwekwa mnamo 2015-04-12.  Check date values in: |date= (help)
  2. "Toothpaste overdose". National Library of Medicine. National Institutes of Health. Iliwekwa mnamo 7 February 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. The History of Toothpaste and Toothbrushes. Bbc.co.uk. Retrieved on April 4, 2013.
  4. "MSNBC: Throw away Chinese toothpaste, FDA warns". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-11-13. Iliwekwa mnamo December 23, 2007.  Check date values in: |accessdate= (help)

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: