Mswaki
Jina hilo ina linaweza kutumiwa tofauti angalia Miswaki (kata ya Uyui)
Mswaki (kutoka Kiarabu سواك, miswaq) ni kifaa cha kusafishia meno, ulimi na ngozi ndani ya mdomo.
Mswaki asilia
haririKimapokeo mswaki ni kijiti kibichi ambacho kinatokana na mti au kichaka na kisha kutafunwa upande mmoja kinatumika kusafishia meno kutoka mabaki ya chakula yanayoweza kuharibu meno.
Hasa ukitokana na mti mswaki (Salvadora persica) (arak kwa Kiarabu) au miti mingine maalumu kadiri ya mazingira, kwa mfano msega au mkupa (Dobera glabra na D. loranthifolia), una sifa za muda mrefu zinazoufanya uendelee kuwa mbadala wa miswaki ya kisasa, ikiwepo ile inayotumia umeme.
Inasemekana mswaki unaimarisha ufizi (nyama inayoshikili meno), unazuia uozo wa meno, unaondoa maumivu ya meno na harufu mbaya kinywani.
Uenezi
haririUnatumika hasa Uarabuni, Afrika Kaskazini, kwenye Sahel na Pembe ya Afrika, India, Asia ya Kati, Asia ya Kusini Mashariki.
Sayansi inasemaje
haririWorld Health Organization (kifupi WHO, yaani Shirika la Afya Duniani chini ya Umoja wa Mataifa) ilihamasisha matumizi ya mswaki mwaka 1986.
Mwaka 2000 ripoti ya kimataifa kuhusu usafi wa kinywa ilionyesha makubaliano ya kwamba unahitajika utafiti zaidi kuthibitisha faida ya mswaki.[1]
Siku hizi watu wengi hutumia miswaki ya kisasa iliyotengenezwa kiwandani yenye shikamano, kichwa na nywele ngumu, kwa kawaida yote ya plastiki, pamoja na dawa ya meno. Utafiti wa mwaka 2003 ulionyesha kwamba matumizi sahihi ya mswaki asili yalikuwa na manufaa kuliko miswaki ya kisasa.[2] Hata hivyo, utafiti uliishia kupima watu 15 tu, idadi isiyotosha kabisa kama uthibitisho wa kisayansi.
Matumizi
haririIngawa wengi wanapiga mswaki hasa asubuhi wanapooga au kunawa, halafu pengine huenda wakanywa chai ambayo inaacha sukari katika meno na hivyo kuandaa uozaji wake, utaratibu sahihi ni kupiga mswaki baada ya chakula, hasa cha jioni, kusudi meno yabaki safi muda wote wa usiku.
Kwa kulinda usafi, ncha ya mswaki inatakiwa kukatwa kila unapotumika.
Usitunzwe kamwe karibu na choo au sinki.
Mswaki ukikauka unatakiwa kulainishwa kwa maji ya waridi.
Katika Uislamu
haririUna nafasi muhimu vilevile katika sheria za Uislamu[3] kutokana na hadithi mbalimbali kusimulia kwamba Mtume Muhammad alikuwa anausifu:[4][5]
Tanbihi
hariri- ↑ "Undersøkelse av en aktuell eldgammel munnrengjøringsmetode". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-05. Iliwekwa mnamo 2015-04-12.
- ↑ Al-Otaibi M, Al-Harthy M, Soder B, Gustafsson A, Angmar-Mansson B. (2003). "Comparative effect of chewing sticks and toothbrushing on plaque removal and gingival health". Oral Health Prev Dent. 1 (4): 301–7. PMID 15643758.
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-08-09. Iliwekwa mnamo 2015-04-12.
- ↑ "Miswak" at sunnah.com.
- ↑ "Siwak" at searchtruth.com.
Marejeo
hariri- Islamic Research on Miswak (Dr. Al Sahli) Archived 20 Aprili 2015 at the Wayback Machine.
- Khan, Tehmeena, Toothbrush (Miswak), in Muhammad in History, Thought, and Culture: An Encyclopedia of the Prophet of God (2 vols.), Edited by C. Fitzpatrick and A. Walker, Santa Barbara, ABC-CLIO, 2014.
Viungo vya nje
hariri- Article on Miswak
- Miswak Is Ecological
- The Miswaak Page - Guidelines and Information Archived 22 Desemba 2010 at the Wayback Machine.
- IslamWeb
- Al Khair - Miswak Archived 25 Novemba 2021 at the Wayback Machine.
- Al-Badr Collection - Miswak Archived 10 Februari 2015 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mswaki kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |