Dayron Robles (alizaliwa Guantanamo, Cuba, 19 Novemba 1986) ni mwanariadha wa kuruka viunzi ambaye anashikilia rekodi ya mbio ya 110m ya kuruka viunzi kwa muda wa sekunde 12.87.Aliweka rekodi hii mnamo 12 Juni 2008 katika mashindano ya Golden Spike Ostrava na yeye ndiye Bingwa wa Olimpiki wa sasa.

Rekodi za medali

Robles akiongoza katika fainali ya mbio ya 110m ya urukaji viunzi katika Olimpiki ya Beijing ya 2008
Riadha ya Wanaume
Anawakilisha nchi Cuba
Michezo ya Olimpiki
Dhahabu 2008 Beijing 110 m ya urukaji viunzi
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Ndani ya Ukumbi
Fedha 2006 Moscow 60 m urukaji viunzi

Wasifu

hariri

Katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Ndani jijini Moscow,alichukua nafasi ya pili kwa muda bora wa kibnafsi(mbio za ndani) wa 7.46s,muda huu ameuboresha sasa ukawa 7.33s(huu ndio muda wa kasi wa pili duniani katika mbio hii ,akiwa nyuma ya Colin Jackson).

Katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2008 mjini Valencia,hakuhitimu kuingia fainali kwa sababu alisimama alipodhani kuwa mwanariadha mwenzake,Liu Xiang alikuwa ameanza mbele ya wengine. Hii ilikuwa bahati mbaya sana kwa Robles,aliyekuwa amekimbia muda tisa kati za muda 11 kasi kabisa katika msimu huo na alikuwa akionekana ni kama atashinda medali ya dhahabu.

Katika michezo ya Olimpiki ya Beijing katika mwaka wa 2008, watu walitarajia mashindano makali kati ya Robles na Liu katika fainali.Liu alishindwa kuendelea baada ya kupata jeraha katika mbio ya kuhitimu kutokana na tendinitis. Robles alishinda fainali kwa urahisi sana kwa muda wa 12.93s na kushinda medali ya dhahabu.

Katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2009,Robles alitoka na hakumaliza mbio za nusu fainali kwa sababu ya jeraha la misuli.

Mafanikio

hariri

Muda bora wa binafsi

hariri
Mashindano Muda (sekunde) Pahali pa kushindana Tarehe
50 m urukaji viunzi 6.39 Stockholm, Uswidi 21 Februari 2008
60 m urukaji viunzi 7.33 Düsseldorf, Ujerumani 8 Februari 2008
110 m urukaji viunzi 12.87 rekodi ya dunia katika mbio hii hadi sasa Ostrava, Czech 12 Juni 2008

Katika Mashindano

hariri
Mwaka Shindano Pahali pa Kushindana Matokeo Mbio ya
2003 Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Vijana Sherbrooke, Kanada 6 110 m urukaji viunzi
2004 Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Vijana ya 2004 Grosseto, Uitalia 2 110 m urukaji viunzi
2005 Mashindano ya Mabingwa wa Amerika ya Kati na Visiwa vya Carribean Nassau, Bahamas 2 110 m urukaji viunzi
2006 Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Ndani ya Ukumbi ya 2006 Moscow, Urusi 2 60 m urukaji viunzi, 7.46 s
Michezo ya Amerika ya Kati na Visiwa vya Carribean ya 2006 Cartagena, Colombia 1 110 m urukaji viunzi, 13.12 s
2007 Michezo ya PanAmerika Rio de Janeiro, Brazili 1 110 m urukaji viunzi, 13.25 s
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia Katika Riadha ya 2007 Osaka, Ujapani 4 110 m urukaji viunzi, 13.15 s
Mashindano ya Dunia ya Riadha ya Fainali ya IAAF ya 2007 Stuttgart, Ujerumani 1 110 m urukaji viunzi, 12.92 s
2008 Mashindano ya Golden Spike Ostrava, Czech 1 110 m urukaji viunzi, 12.87 s
Olimpiki ya 2008 Beijing, Uchina 1 110 m urukaji viunzi, 12.93 s

Marejeo

hariri
  1. "World Indoor Championship Results".
  2. "Liu Xiang to meet Robles in World Champs".
  3. Frederik Balfour (August 18, 2008). "China Olympic Hero Liu Xiang Quits Games". BusinessWeek.
  4. "Merritt of U.S., Cuba's Robles capture track gold".
  5. "Robles, Dayron biography". IAAF. Ilihifadhiwa 5 Agosti 2011 kwenye Wayback Machine.

Viungo vya nje

hariri
Alitanguliwa na
Liu Xiang
Wanaume walioshikilia rekodi ya 110m ya urukaji viunzi
12 Juni 2008 –
Akafuatiwa na
Yeye ndiye Bingwa Mtetezi
Alitanguliwa na
Liu Xiang
Mwanaume Bora wa mbio ya 110m ya Urukaji viunzi wa mwaka
2007 (akiwa pamoja na Liu Xiang), 2008
Akafuatiwa na
Yeye ndiye Bingwa Mtetezi
Alitanguliwa na
Asafa Powell
IAAF Mtendaji bora wa mwaka
2008
Akafuatiwa na
Yeye ndiye Bingwa Mtetezi