Brazil

(Elekezwa kutoka Brazili)


Brazil ni nchi kubwa ya Amerika ya Kusini na pia ni nchi yenye wakazi wengi kushinda nchi zote za bara hilo. Eneo lake ni karibu nusu ya bara lote.

República Federativa do Brasil
Shirikisho la Jamhuri ya Brazil
Bendera ya Brazil Nembo ya Brazil
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Ordem e Progresso
(Kireno kwa "Utaratibu na Maendeleo")
Wimbo wa taifa:
Ouviram do Ipiranga as margens plácidas
("Kando ntulivu za Ipiranga zilisikia...")
Lokeshen ya Brazil
Mji mkuu Brasília
15°45′ S 47°57′ W
Mji mkubwa nchini São Paulo
Lugha rasmi Kireno
Serikali Shirikisho la Jamhuri
Jair Bolsonaro
Uhuru
Ilitangazwa
Ilitambuliwa
Jamhuri

7 Septemba 1822
29 Agosti 1825
15 Novemba 1889
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
8,515,767 km² (ya 5)
0.65
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
202,768,562 (ya 5)
169,799,170
23.8/km² (ya 182)
Fedha Real (BRL)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-2 to -5 (Official: -3))
(UTC)
Intaneti TLD .br
Kodi ya simu +55

-


Imepakana na Uruguay, Argentina, Paraguay, Bolivia, Peru, Kolombia, Venezuela, Guyana, Surinam na eneo la Guyana ya Kifaransa.

Brazil ina pwani ndefu kwenye bahari ya Atlantiki.

Mji mkuu ni Brasilia, uliopangwa na kujengwa kati ya 1957 na 1960. Mji mkubwa ni Sao Paulo.

JiografiaEdit

Misitu mipana ya dunia inapatikana Brazil katika beseni ya mto Amazonas. Misitu hii inafunika takriban 40% ya eneo la nchi.

Idadi kubwa ya wakazi hukalia maeneo karibu na pwani ya Atlantiki.

Kitovu cha kilimo ni nyanda za "cerado" au savana katika magharibi ya kati ya Brazil.

MilimaEdit

 
Mlima wa Corcovado na sanamu ya Yesu Mwokozi (Rio de Janeiro)

Mlima mkubwa ni Pico da Neblina (mita 3,014 juu ya UB) pamoja na Pico 31 de Março (mita 2,992) ulio karibu nao kwenye mipaka ya Brazil, Venezuela na Guyana.

Mlima mkubwa wa kusini ni Pico da Bandeira (mita 2.891).

Mlima unaojulikana zaidi si mkubwa lakini uko ndani ya mji wa Rio de Janeiro: ni Corcovado wenye mita 710. Juu yake kuna sanamu ya Yesu Kristo ambayo ni ishara ya mji.

Mito muhimuEdit

 
Ramani ya mwendo wa Amazonas inayovuka bara lote.

Brazil ina mto mkubwa na mrefu wa dunia ambayo ni Amazonas wenye urefu wa takriban kilometa 7000. Matawimto yake muhimu ni Río Purús, Rio Negro na Rio Tapajós.

Katika mashariki kuna mto Iguaçu wenye maporomoko ya Iguaçu ambayo ndiyo makubwa duniani.

 
Maporomoko ya Iguaçu karibu na mpaka wa Argentina/Brazil/Paraguay
 
Fortaleza

Parana (3.998 km) ni mto mrefu duniani baada ya Amazonas. Unalisha kituo kikubwa cha nishati ya maji duniani cha Itaipú.

Lagoa dos Patos karibu na Porto Alegre ni wangwa kubwa la Brazil lenye 10.000 km².

Ipiranga si mto mkubwa, hata kama jina lake linapatikana katika wimbo wa taifa.

VisiwaEdit

Brazil ina visiwa vichache vidogo katika Atlantiki kama vileː

Visiwa hivyo ni sehemu ya mgongo kati wa Atlantiki; hali halisi ni vilele vya milima inayoanza kwenye msingi wa bahari.

Kisiwa kikubwa cha Brazil hakipo baharini bali kati ya mto Amazonas: ni Marajó, chenye eneo la km² 48.000 (kubwa kushinda eneo la Uswisi).

Hali ya hewaEdit

Hali ya hewa ni ya kitropiki isipokuwa kusini.

Beseni ya Amazonas ina mvua nyingi. Kwenye milima ya kusini usimbishaji unaweza kutokea kama theluji.

Miji muhimuEdit

 
São Paulo inazidi wakazi milioni 20
 
Rio de Janeiro
 
Curitiba, kusini mwa Brazil

Jiji kubwa ni São Paulo linalofikia (pamoja na mitaa ya jirani) kwenye idadi ya wakazi milioni 20.5.

Majiji ya kufuata ni Rio de Janeiro (wakazi milioni 11.4), Belo Horizonte (wakazi milioni 4.3), Curitiba (wakazi milioni 4), Recife (wakazi milioni 3.6), Brasilia (wakazi milioni 2.9), Salvador da Bahia (wakazi milioni 2.9), Fortaleza (wakazi milioni 2.6).

São Paulo ni jiji kubwa kabisa linalokua haraka sana. Ni moyo wa uchumi wa Brazil wenye viwanda vingi.

Rio de Janeiro ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi kuanzishwa kwa Brasilia. Imejulikana kote duniani kutokana na uzuri wa mazingira yake na sherehe ya Kanivali. Ina pia viwanda muhimu na ni kitovu cha utamaduni wa nchi.

Mji mkuu wa Brasilia ulijengwa kama ishara ya umoja wa nchi katika miaka mitatu tu.

Jumla ya asilimia 70 za wakazi hukalia miji mikubwa. (Angalia Orodha ya miji ya Brazil.)

HistoriaEdit

Brazil imekaliwa na watu tangu miaka 10,000 iliyopita. Waindio waliingia kutoka kaskazini. Hakuna taarifa za kimaandishi lakini akiolojia imeweza kufumbua makazi mbalimbali ya wenyeji asilia.

UkoloniEdit

Brazil ilikuwa koloni la Ureno hadi mwaka 1822 kutokana na mkataba wa Tordesillas ambamo Hispania na Ureno zilipatana tarehe 5 Septemba 1494 kuhusu ugawaji wa dunia kati yao baada ya fumbuzi za Kolumbus.

Mreno wa kwanza aliyefika mwambao wa Brazil tarehe 22 Aprili 1500 alikuwa Pedro Alvares Cabral. Makazi ya kwanza ya Wareno ni mji wa São Vicente mwaka 1532. Mji mkuu wa kwanza ulikuwa bandari ya Salvador da Bahia tangu 1549.

Wareno walianzisha kilimo cha miwa wakiwalazimisha Waindio kuwafanyia kazi. Walianza kuingia ndani ya bara wakitafuta watumwa kwa ajili ya mashamba na dhahabu.

Hali ya WaindioEdit

Wenyeji walipungua haraka kwa sababu ya kuambukizwa magonjwa ya kigeni wakikosa kinga dhidi yake, halafu kutokana na kutendewa vibaya kama watumwa mashambani.

Wareno walianza kutafuta wafanyakazi penginepo kwa kuchukua watumwa kutoka Afrika.

Mapadri WajesuitiEdit

Katika hali hiyo wamisionari Wakristo wa Shirika la Yesu walisimama upande wa Waindio. Walijipatia tamko rasmi la Papa wa Roma la kuwa Waindio ni binadamu kamili, hivyo hawafai kutendewa kinyama. Wakibatizwa na kuwa Wakristo walitakiwa kukubaliwa kama raia yeyote wa Ureno – amri ambayo mara nyingi haikukubaliwa na wavindaji wa watumwa na wenye mashamba.

Mapadri wa Shirika la Yesu walianzisha „reduciones“ yaani vijiji na miji kwa ajili ya Waindio walioishi chini ya ulinzi wao na kutetewa dhidi ya wavindaji wa watumwa. Katika makazi hayo Waindio walifundishwa shule kwa lugha za kienyeji na Kireno, na kupata mafunzo wa ufundi mbalimbali. Kwa namna hiyo mapadri hao walitawala maeneo makubwa ndani ya bara.

Hali hiyo ilisababisha hasira ya wanasiasa Wareno walioendelea kuwapinga hadi Ureno penyewe. Hatimaye mwaka 1767 hao mapadre Wajesuiti walilazimishwa kuondoka katika Ureno na makoloni yake yote.

Upanuzi wa BrazilEdit

Karne ya 17 na ya 18 iliona kuanzishwa kwa miji mizuri kwa sababu dhahabu na almasi zilivumbuliwa katika misitu ya beseni ya Amazonas. Misafara ya kutafuta hazina hizi zilipanua eneo la Brazil kuelekea magharibi.

Mji mkuu ulihamishwa kwenda Rio de Janeiro mwaka 1763.

Uhuru 1822Edit

Uhuru wa Brazil ulisababishwa na siasa za Ulaya. Mwaka 1807 Ureno ilivamiwa na Ufaransa ya Napoleon Bonaparte. Mfalme wa Ureno João VI alikimbilia Brazil, Rio de Janeiro ikawa mji mkuu wa dola la Ureno.

Mfalme aliporudi Ureno mwaka 1821 alimwachia mtoto wake Pedro utawala wa Brazil. Mwaka 1822 Pedro aliyeona mabadiliko ya kimapinduzi katika makoloni ya Hispania kote Amerika ya Kusini aliamua kutangaza uhuru wa Brazil akiwa mwenyewe mfalme kwa cheo cha Kaisari.

WatuEdit

Kutokana na historia ya nchi, wakazi wengi wana asili ya Ulaya (47.7%) au ni machotara (43.1). Asilimia 7.6 wana asili ya Afrika tu.

Wakazi walio wengi hutumia lugha ya Kireno, lakini kuna lugha nyingi kwa sababu ya vikundi vya wenyeji asilia (Waindio) na wahamiaji kutoka pande zote za dunia.

Asilia 64.6 ya wananchi wanafuata imani ya Kanisa Katoliki. Ndiyo nchi yenye Wakatoliki wengi kuliko zote duniani. Waprotestanti ni asilimia 22.2.

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyana ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

  Makala hii kuhusu maeneo ya Brazil bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Brazil kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.