Kipanya-kinamasi
Kipanya-kinamasi | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Msambazo wa kipanya-kinamasi
|
Kipanya-kinamasi (Delanymys brooksi) ni mnyama mgugunaji mdogo na spishi pekee ya nusufamilia Delanymyinae katika familia Nesomyidae. Anatokea vinamasi na maeneo manyevu mengine ya mwinuko mkubwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.
Maelezo
haririHuyu ni kipanya mdogo sana. Ana urefu wa sm 5-6 tu na uzito wa g 5-7. Mkia wake ni mrefu sana kuwiana na ukuwba wake na ni sm 9-11. Una manyoya machache sana lakini una vigamba katika ruwaza ya miviringo. Manyoya ni marefu (mm 8-10), kahawianyekundu au hudhurungi juu na njano iliyofifia chini. Manyoya meusi marefu zaidi yamesambaa katikati ya mengine. Kuna manyoya meupe yaliyozunguka kitundu cha kukojoa na kuzaa, na baka jeupe kwenye koo. Manyoya meusi mafupi yanazunguka macho na kuna baka jeusi kati ya macho na ncha ya pua. Kuna sekini za manyoya meupe kwenye kila kifundo cha mkono ambazo hufikiriwa kuwa na kazi ya kugusa.
Nyayo za nyuma ni ndefu pia (zaidi ya sm 1) na vidole 2-5 vya miguu yote ni virefu, 3 na 4 zaidi kuliko 2 na 5. Vinabeba kucha ndefu zilizopindika. Vidole vya kwanza vya miguu ya mbele ni vidogo sana na vinabeba kucha ndogo tu. Chini ya nyayo na ya vidole kuna vinundu vingi. Hiyo yote inazaidia vipanya kupanda nyasi na mimea ingine. Vidole vinaweza kutandwa vipana ili kupanda juu na kubanwa ili kuzuia kuteleza chini kwa mmea. Mkia mrefu wenye uwezo wa kushikilia hutumiwa kupea usawaziko wakati wa kupanda na ncha inaweza kuviringania shina ili kupea egemeo.
Kipanya huyo hula mbegu hasa.