Do You
"Do You" ni wimbo wa 2007 ulioimbwa na mwimbaji-mtunzi wa R&B Ne-Yo. Wimbo unamzungumzia Ne-Yo akiwa anajaribu kumwuliza mwanamke wake wa zamani kuwa keshawahi kumfikiria kabisa. Ni wimbo wa pili kutoka katika albamu yake ya pili ya Because of You.
“Do You” | ||
---|---|---|
Kasha ya wimbo wa Do You
| ||
Single ya Ne-Yo kutoka katika albamu ya Because of You | ||
Imetolewa | 12 Juni 2007/24 Julai (USA), 2007 (Ufalme wa Muungano), 30 Julai 2007 (Ujapani), 21 Novemba 2007 (akimsh. Utada) | |
Muundo | Radio Airplay/CD single, 12" single | |
Imerekodiwa | 2007 | |
Aina | R&B, pop | |
Urefu | 3:48 | |
Studio | Def Jam Recordings | |
Mtunzi | Allen, M./Smith, S./Sparkman, M. | |
Mtayarishaji | The Heavyweights | |
Single za Ne-Yo na tarehe zake | ||
"Because of You" (2006) |
"Do You" (2007) |
"Can We Chill" (2007)
|
Single za Utada na tarehe zake | ||
"Beautiful World / Kiss & Cry" (2007) |
"Do You" (2007) |
"Heart Station / Stay Gold" (2008) |
Wimbo ulitolewa rasmi katika maredio kunako tarehe 12 Juni 2007. Katika mahojiano yake na BET, Ne-Yo amesema kwamba wimbo wa "Do You" ni sehemu ya pili ya wimbo wake wa awali wa "So Sick" ambao unatoka katika albamu yake ya kwanza ya In My Own Words.[1]
Remix ya wimbo huu amemshirikisha mwanamama Mary J. Blige. Na remix yake nyingine amepata kumshirikisha mwanadada mwingine aitwaye Hikaru Utada, ambao ulitolewa nchini Japan kunako 21 Novemba 2007 ikiwa kama mmoja kati ya wimbo wa 7 kwa tungo zake za Kiingereza kutoka kwa mwanadada huyo.
Video yake
haririMwanzoni kabisa Ne-Yo anaonekana akipigana na mpenzi wake wa zamani katika gari, ambaye baadaye aliondoka zake. Ne-Yo akawa anajaribu kuandika barua kwa mpenzi wake huyo huku akiwa anajaribu kumwuliza kama ana mkumbuka.
Inaonekana kuwa ni vigumu kwa yeye kumkumbuka, na baadaye akapata kusoma barua aliyotumiwa na Ne-Yo na akaamua kuikunja-kunja na kuitupilia mbali. Mpenzi huyo baada ya muda anaonekana kumpiga busu mpenzi wake mpya wakiwa katika kochi, na akiwa amemlalia mapajani, wakati huohuo akiwa amemkalia mbali kidogo.
Ne-Yo kisha akakumbuka sehemu ambayo alikuwa ana kawaida ya kumpiga busu mpenzi wake huyo katika kochi hilohilo alilokaa na huyo bwana mpya. Ne-Yo akaonekana akiendesha gari kwa kasi kisha akalisimamisha katika eneo lenye kibanda cha kupigia simu za kulipia, na kuanza kumpigia simu mpenzi wake wa zamani aje katika eno lile la kibanda cha simu za kulipia. Lakini kwa kwa bahati mbaya ule muda ambao dada yeye kafika, Ne-Yo yeye akawa tayari kesha ondoka zake.
Chati
haririChati (2007) | Nafasik Iliyoshika |
---|---|
Brazil Hot 100 | 14 |
U.S. Billboard Hot 100 | 26 |
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs | 3 |
U.S. Billboard Pop 100 | 86 |
Official UK Singles Chart | 100 [2] |
Remix aliyoimba na Hikaru Utada
haririMauzo ya Digital na Chati za Ujapani
haririChati | Nafasi iliyoshika |
---|---|
Nyimbo za iTunes za Ujapani | #1 |
Recochoku Chaku-Uta Downloads[3] | #1 |
Recochoku Chaku-Uta Full[4] | #1 |
Marejeo
hariri- ↑ "New UK Single Releases, New Music Releases, UK CD Single Releases". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-02. Iliwekwa mnamo 2008-09-26.
- ↑ "ChartStats.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-30. Iliwekwa mnamo 2007-09-30.
- ↑ (Kijapani) 「着うたフル®」・「着うた®」なら「レコ直♪」 - 「着うた®」ダウンロードランキング Archived 19 Juni 2012 at the Wayback Machine.
- ↑ (Kijapani) 「着うたフル®」・「着うた®」なら「レコ直♪」 - 「着うたフル®」ダウンロードランキング Archived 18 Machi 2011 at the Wayback Machine.