Dolar (pesa)
,
Dolar (pia dola, Kiing. dollar) ni jina la pesa ya Marekani na nchi mbalimbali duniani.
Dola ya Marekani au US-Dollar ndiyo inayojulikana zaidi, lakini kuna nchi zaidi ya 20 zinazotumia neno "Dollar" kwa pesa yao.
Nchi zenye pesa inayoitwa "Dollar" (dola)
haririHistoria
haririAsili ya jina hilo ni neno la Kijerumani "taler" (au: thaler) kwa ajili ya sarafu ya fedha iliyotolewa kwenye mji wa Joachimsthal kule Bohemia (Ucheki) mnamo mwaka 1518.
Wakati ule migodi ya Joachimsthal ilikuwa na fedha nyingi kiasi kwamba mji ulianza kutoa pesa zake. Pesa hizo zilitwa (kufuatana na mji) "Joachimsthaler", iliyofupishwa kuwa "taler" tu.
Taler ilikuwa pesa iliyopendwa sana Ulaya ikasambaa kote.
Hispania ilitumia jina hilo kwa "dolaro" yake kuanzia mwaka 1575. Dolaro ya Hispania ilikuwa baadaye pesa ya kisheria ya Marekani ilipojitenga na Uingereza na kuanzisha pesa yake mwaka 1792.