Ucheki
Ucheki au Chekia au Czechia (kwa Kicheki: Česko) pia Jamhuri ya Kicheki au Jamhuri ya Czech (kwa Kicheki: Česká republika) ni nchi ya Ulaya ya Kati na mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Pravda vítězí (Kicheki: "Ukweli hushinda") | |||||
Wimbo wa taifa: Kde domov můj | |||||
Mji mkuu | Praha | ||||
Mji mkubwa nchini | Praha | ||||
Lugha rasmi | Kicheki | ||||
Serikali | Jamhuri Petr Pavel Petr Fiala | ||||
' Kutokea kwa taifa Uhuru kutoka Austria-Hungaria Mwisho wa Chekoslovakia |
Karne ya 9 (Dola la Moravia) 28 Oktoba 1918 1 Januari 1993 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
78,866 km² (ya 117) 2.0 | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2021 sensa - Msongamano wa watu |
10,827,529 (ya 85) 10,524,167 133/km² (ya 91) | ||||
Fedha | Koruna (CZK )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .cz 3 | ||||
Kodi ya simu | +4201
|
Imepakana na Poland, Ujerumani, Austria na Slovakia.
Mji mkuu ni Praha (Kijer.: Prag; Kiing.: Prague).
Miji mingine mikubwa ni Brno, Ostrava, Zlín, Plzeň, Pardubice, Hradec Králové, České Budějovice, Liberec, Olomouc na Ústí nad Labem.
Tangu zamani nchi imekuwa na kanda za Bohemia, Moravia na Silesia.
Wakazi husema hasa Kicheki ambacho ni lugha ya Kislavoni ya Magharibi.
Ni kati ya nchi ambako dini si muhimu kimaisha. Wakati wa sensa ya mwaka 2021, 56.9% ya wakazi walisema hawana dini yoyote, 30.1% hawakujibu swali husika, 11.7% walijitambulisha kama Wakristo (Wakatoliki 9.3% na madhehebu mengine 2.4%).
Historia
haririMapema zaidi nchi ilikuwa ufalme wa Moravia kuu katika karne ya 7.
Historia ya jamhuri ya Ucheki yenyewe si ndefu, tukiangalia tangu nchi hiyo kupokea uhuru kamili mwaka 1993 hadi leo.
Hapo awali Ucheki ilikuwa imeungana na Slovakia wakiwa Cheko-Slovakia (Czechoslovakia) ambayo tena ilikuwa kwanza chini ya utawala wa ufalme wa Austro-Hungaria katika karne ya 19 hadi mwanzo wa karne ya 20, yaani mpaka vita kuu ya kwanza ya dunia wakati ufalme uliposhindwa na kusambaratika.
Rais wa kwanza kuteuliwa kwa taifa hilo mpya ni Tomáš Garrigue Masaryk.
Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia Wajerumani walichukua uongozi wa Chekoslovakia, lakini hawakudumu mno.
Kufikia mwisho wa vita hivyo USSR ilichukua unahodha na kuweka nchi hiyo katika sera ya Ukomunisti.
Wananchi walitawaliwa kwa nguvu halisi hadi mwaka 1989 wakati kulitokea mapinduzi ya amani na kupata uhuru halisi na demokrasia.
Mwaka 1993, nchi hiyo iligawanyika katika Ucheki na Slovakia kwa sababu ya kisiasa.
Mwaka 1999 nchi ya Ucheki ilijiunga na NATO.
Ucheki imekuwa mwanachama wa muungano ya Umoja wa Ulaya kuanzia mwaka 2004.
Ucheki ni maarufu katika dunia kwa usalama wake na inapendwa sana na mamilioni ya watalii ambao huizuru kila mwaka.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Picha za Ucheki Ilihifadhiwa 5 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
- Ramani ya Ucheki Ilihifadhiwa 21 Desemba 2004 kwenye Wayback Machine.
- Ramani ya Ucheki - staili ya Google Maps
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ucheki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |