Dominique Anglade (alizaliwa Januari 31, mwaka 1974) ni mfanyabiashara na mwanasiasa wa nchini Kanada ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa chama cha Kiliberali cha Quebec na kiongozi wa Upinzani wa Quebec kuanzia Mei 11, 2020 hadi Desemba 1, 2022. [1]

Dominique Anglade

Dominique alihudumu kama mjumbe wa Bunge la Kitaifa la Quebec kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2022, akiwakilisha jimbo la Saint-Henri-Sainte-Anne.

Dominique ni mwanamke wa kwanza kuongoza Chama cha Kiliberali cha Quebec, na pia mwanamke wa kwanza mweusi kuongoza jimbo nchini Kanada. Mbali na hayo, Dominique ni mtu wa kwanza mwenye asili ya Haiti kuwa waziri wa baraza la mawaziri nchini Kanada. Dominique ni binti wa msomi Georges Anglade .

Pia aliwahi kuwa mwanamke wa kwanza kushika ngazi ya mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya kiuchumi iitwayo Montreal International.

Marejeo

hariri
  1. Antoni Narestant, "Dominique Anglade quits as leader of Quebec Liberal Party". CBC News Montreal, November 7, 2022.
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dominique Anglade kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.