Haiti ni nchi kwenye kisiwa cha Karibi cha Hispaniola. Eneo la Haiti ni takriban theluthi moja ya Hispaniola yote. Sehemu kubwa ya kisiwa inaunda nchi jirani ya Jamhuri ya Dominika.

Jamhuri ya Haiti
Krioli: Repiblik d Ayiti
Kifaransa: République d'Haïti'
Bendera ya HaitiF Nembo ya HaitiF
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: L'Union Fait La Force
("Umoja ni nguvu")
Wimbo wa taifa: La Dessalinienne
Lokeshen ya HaitiF
Mji mkuu Port-au-Prince
18°32′ N 72°20′ W
Mji mkubwa nchini Port-au-Prince
Lugha rasmi Kifaransa na Krioli ya Haiti
Serikali Jamhuri
Claude Joseph
Ariel Henry
Uhuru
kutoka Ufaransa
1 Januari 1804
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
27,750 km² (ya 147)
0.7
Idadi ya watu
 - Julai 2018 kadirio
 - 1982 sensa
 - Msongamano wa watu
 
11,439,6461 (ya 85)
5,053,792
382/km² (ya 32)
Fedha Gourde (HTG)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-5)
(UTC-4)
Intaneti TLD .ht
Kodi ya simu +509

-


Ramani ya Haiti

Haiti ni nchi ya kwanza duniani ambako watumwa wenye asili ya Afrika walifaulu kukomesha utumwa na kujipatia uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1804.

Haiti ni kati ya nchi maskini kabisa duniani na nchi maskini zaidi katika Amerika yote.

Mji mkuu ni Port-au-Prince.

Jiografia hariri

Jina la "Haiti" lina asili katika lugha ya Kitaino ya wakazi asilia; linamaanisha "nchi ya milima", na kweli kisiwa kina milima mingi.

Nchi imegawanywa katika wilaya kumi.

Historia hariri

Mwanzo na ukoloni wa Hispania hariri

Wakazi asilia walikuwa Waindio Waarawak.

Baada ya kufika kwa Kristoforo Kolumbus na utawala wa Hispania idadi yao ilipungua haraka kutokana na magonjwa ya Ulaya ambayo hawakuzoea na kukosa kinga dhidi yake, lakini pia kutokana na kutendwa kwa unyama na mabwana wapya.

Wahispania walianzisha mashamba kwa kutegemea kazi ya watumwa kutoka Afrika.

Mnamo mwaka 1600 Waindio wachache tu walibaki kutoka malakhi wakati wa Kolumbus wakapotea kabisa kwa njia ya kuoa au kuolewa na Wazungu na Waafrika.

Ukoloni wa Ufaransa hariri

Katika karne ya 17 Wafaransa walifika kisiwani wakanunua theluthi moja ya kisiwa wakaiita "Saint-Domingue" kilichokuwa baadaye Haiti. Wafaransa walileta watumwa wengi kutoka Afrika na kujenga uchumi wa mashamba makubwa, hasa ya miwa. Koloni la Saint-Domingue lilikuwa koloni tajiri la Ufaransa katika Amerika.

Mapinduzi ya Ufaransa hariri

Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1789 koloni lilikuwa na wakazi wa aina nne:

  • Wazungu, hasa Wafaransa, waliokuwa mabwana lakini walikuwa na tofauti kubwa kati yao: wengine tajiri sana wengine maskini - jumla takriban watu 32,000
  • machotara na Weusi huru ambao walikuwa raia wa daraja ya pili; wengine walikuwa matajiri na mabwana wa mashamba na pia wa watumwa - jumla watu 28,000
  • watumwa wenye asili ya Kiafrika - jumla watu 500,000
  • Wamaroni walikuwa watumwa wakimbizi walioishi mlimani katika pori - idadi yao haijulikani lakini hawakuwa wengi.

Mapinduzi ya Ufaransa na kutangaziwa kwa haki za kibinadamu vilisababisha matumaini ya machotara wenye mali ya kukubaliwa kama raia kamili wenye haki ya kupiga kura. Wenyewe hawakutegemea kumaliza utumwa uliokuwa msingi wa uchumi. Lakini matumaini yao yalishindikana wakakataliwa na watawala kisiwani.

 
Toussaint L'Ouverture kiongozi wa uhuru wa Haiti

Mapinduzi ya Haiti hariri

Sehemu ya matajiri kati ya Wazungu walitaka kujitenga na Ufaransa kwa msaada wa Uingereza na Hispania wakichukia mapinduzi katika Ufaransa. Watumwa na Weusi huru wenye elimu walifuata habari hizi wakaogopa ya kwamba utawala wa mabwana hao bila sheria za Ufaransa utakuwa mbaya kuliko hali jinsi ilivyokuwa wakaanza mapinduzi.

Kiongozi wao alikuwa Toussaint L'Ouverture aliyefaulu kushika serikali ya koloni tangu mwaka 1798. Awali alipigania jeshi la Ufaransa; baada ya bunge la Paris kutangaza mwisho wa utumwa alishirikiana na Ufaransa dhidi ya jeshi la mabwana wenye mashamba waliotaka kuendeleza utumwa katika nchi ya kujitegemea.

Toussaint L'Ouverture alishinda pia Waingereza waliotaka kuwasaidia wapinzani Wafaransa wa Paris na mwaka 1801 akateka kaskazini mwa kisiwa iliyokuwa eneo la Kihispania na kutawala Hispaniola yote akitangaza kote mwisho wa utumwa.

Lakini mnamo mwaka 1802 siasa ya Paris ilibadilika na mtawala Napoleon Bonaparte aliamua kurudisha Hispaniola katika hali ya awali akatuma jeshi kubwa la askari 40,000. L'Ouverture alikamatwa alipokubali kushauriana na jenerali Mfaransa akapelekwa kama mfungwa Ulaya. Lakini makamu wake Jean-Jacques Dessalines aliposikia kuhusu mipango ya Ufaransa ya kurudisha utumwa alianza vita upya. Katika vita vikali Wafaransa walishindwa na Dessalines alitangaza uhuru wa koloni tarehe 1 Januari 1804 kwa jina la "Haiti" kama "Jamhuri ya watu weusi".

Wilaya za Haiti hariri

 
Wilaya za Haiti
 
MINUSTAH kazini wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2006.
  1. Artibonite (Gonaïves)
  2. Centre (Hinche)
  3. Grand'Anse (Jérémie)
  4. Nippes (Miragoâne)
  5. Nord (Cap-Haïtien)
  6. Nord-Est (Fort-Liberté)
  7. Nord-Ouest (Port-de-Paix)
  8. Ouest (Port-au-Prince)
  9. Sud-Est (Jacmel)
  10. Sud (Les Cayes)

Watu hariri

Wakazi ni 11,439.646 (2018), lakini wananchi wengine wengi wamehama kutokana na ufukara. Karibu 900,000 wako Marekani, 800,000 wako Dominikana na 300,000 Kuba, halafu Kanada, Ufaransa, Bahamas.

Uchunguzi wa DNA umeonyesha kwamba Afrika Kusini kwa Sahara imeichangia 95.5% na Ulaya 4.3%.

Kuna lugha rasmi mbili: moja ni Kifaransa (42%) na nyingine ni Kihaiti ("Kreyol") inayotokana nacho (karibu 100%).

Wakazi wengi ni wafuasi wa Yesu Kristo (86.4%) (katika Kanisa Katoliki 56.8% na madhehebu ya Kiprotestanti 29.6%) lakini wengi hufuata vilevile dini ya vudu inayotokana na dini za jadi kutoka Afrika ya Magharibi.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Haiti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.