Donald Gordon (mfanyabiashara)
Donald Gordon, CC, CMG (11 Desemba 1901 - 2 Mei 1969) alikuwa mfanyabiashara wa Kanada na rais wa zamani wa Shirika la Kitaifa la reli la Kanada (Canadian National Railway - CNR) kutoka mwaka wa 1950 hadi mwaka wa 1966.
Alizaliwa Oldmedrum, Scotland akahamia Kanada akiwa umri mdogo sana. Akiwa umri wa miaka 15,alijiunga na Benki ya Nova Scotia jijini Toronto, kabla ya kuwa naibu wa mhasibu mkuu na naibu wa meneja wa tawi la benki hiyo jijini Toronto. Katika mwaka wa 1935, aliteuliwa kama Katibu wa Benki ya Kanada na akawa naibu wa gavana wa benki hiyo hapo baadaye. Kati ya miaka ya 1941-1947, alikuwa Mwenyekiti wa bodi ya War-Time Prices and Trade Board. Alikuwa mkuu wa Shirika la Kitaifa la reli la Kanada katika miaka ya 1950 - 1966.
Alihusika katika mgogoro mkali wa kuipa jina Hoteli ya Queen Elizabeth ilipoundwa jijini Montreal. Wapenzi wa Quebec walitaka hoteli hiyo iitwe Château Maisonneuve kwa makumbusho ya mwanzilishi wa Montreal,Paul Chomedey de Maisonneuve. Gordon, alisisitiza sana hoteli iitwe jina la Malkia Elizabeth ,ambaye alikuwa amepanda na kuchukua kiti cha utawala kwa ghafla katika mwaka wa 1952. Wakati huu, ndio mipango ya hoteli hiyo ikiwa ikifikiriwa na kuchorwa na wasanii na wataalam.
Katika mwaka wa 1944, yeye alituzwa tuzo ya Amri ya Mtakatifu Michael na Mtakatifu George(Order of St. Michael & St. George). Katika mwaka wa 1968, alipewa tuzo ya Amri ya Kanada (Order of Canada).
Chuo Kikuu cha Queen katika mji wa Kingston, Ontario ilimpa heshima kubwa Gordon ilipoamua kuiita nyumba za makazi ya wanafunzi Donald Gordon House na jumba lao la mikutano likaitwa Donald Gordon Centre. Yeye ni mwanachama wa Ukumbi wa Wafanyibiashara Maarufu wa Kanada.
Viungo vya nje
hariri- Donald Gordon Ilihifadhiwa 7 Juni 2011 kwenye Wayback Machine. katika Kamusi ya Kanada