Bunge la Afrika Mashariki

(Elekezwa kutoka EALA)

Bunge la Afrika Mashariki (kwa Kiingereza: East African Legislative Assembly, kifupi: EALA) ni chombo cha Jumuia ya Afrika Mashariki kwa kutunga sheria. Wabunge wanahudumu kwa miaka mitano.[1]

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akihutubia Bunge.

Bunge lilianzishwa tarehe 30 Novemba 2001.

Bunge la nne lina wajumbe 62, yaani 9 kwa kila nchi mwanachama, wakichaguliwa na bunge la nchi husika namna ya kuwakilisha kweli taifa lote, na wengine 8 kutokana na wadhifa wao. Spika ni Martin Ngoga kutoka Rwanda.

Tanbihi

hariri
  1. "4th Assembly 2017- 2022 —East African Legislative Assembly". www.eala.org. East African Community. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-04. Iliwekwa mnamo 2020-12-04.