Edoardo Prettner Cippico

Edoardo Prettner Cippico (10 Oktoba 19057 Aprili 1983) [1] alikuwa padre Mkatoliki wa Italia na afisa katika Masijala ya Siri ya Vatikani. [2]

Alikamatwa na kufungwa mnamo mwaka 1948 kwa tuhuma za uhalifu wa kifedha, na baadaye alifunuliwa kuwa alifanya ujasusi kwa niaba ya Umoja wa Kisovieti. Skendo ya Cippico ilikuwa aibu kwa Kanisa Katoliki, hasa wakati wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1948, ambapo Umoja wa Kidemokrasia wa Watu, ambao ulikuwa na mwelekeo wa kushoto, ulitoa changamoto kubwa kwa serikali ya Demokrasia ya Kikristo iliyohusiana na Kanisa Katoliki.[3][4]

Marejeo

hariri
  1. "Cronaca contemporanea 26 febbraio–10 marzo 1948; I Santa Sede; 5 Lo scandalo Prettner Cippico". La Civiltà Cattolica (kwa Kiitaliano). I Anno 99 (2346): 656. 20 Machi 1948.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Priest Imprisoned at Vatican in 1948 Dies", Catholic News Service, 11 April 1983, p. 7. (English) 
  3. Domenico, Roy (10 Septemba 2021). The Devil and the Dolce Vita: Catholic Attempts to Save Italy's Soul, 1948–1974 (kwa Kiingereza). CUA Press. uk. 85. ISBN 978-0-8132-3433-5. JSTOR j.ctv1z2hmtv.6. Kigezo:Project MUSE.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Le truffe di don Cippico", La Repubblica, 27 March 1998. (it) 
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.