Egidio Lari (8 Machi 188217 Novemba 1965) alikuwa prelati wa Italia katika Kanisa Katoliki aliyefanya kazi katika huduma ya kidiplomasia ya Vatikani. Egidio Lari alizaliwa huko Buggiano, katika Jimbo la Pistoia, Italia, tarehe 8 Machi 1882. Alipadrishwa kuwa kuhani tarehe 18 Septemba 1909.

Mnamo tarehe 29 Juni 1931, Papa Pius XI alimteua kuwa askofu mkuu wa heshima (titular archbishop) na Mjumbe wa Kitume kwenda Iran.[1] Alipokea daraja ya uaskofu tarehe 15 Agosti kutoka kwa Kardinali Luigi Sincero. Alirudi Roma mnamo Machi 1936.

Tarehe 11 Mei 1939, Papa Pius XII alimteua kuwa Balozi wa Kitume (Apostolic Nuncio) nchini Bolivia.[2] Alistaafu kutoka wadhifa huo tarehe 3 Januari 1945. Alifariki dunia tarehe 17 Novemba 1965 akiwa na umri wa miaka 86.

Marejeo

hariri
  1. Acta Apostolicae Sedis (PDF). Juz. la XXIV. 1932. uk. 102. Iliwekwa mnamo 26 Agosti 2019.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Acta Apostolicae Sedis (PDF). Juz. la XXXI. 1939. uk. 233. Iliwekwa mnamo 26 Agosti 2019.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.