Einsteini

(Elekezwa kutoka Einsteinium)

Einsteini (Einsteinium) ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 99. Hiyo inamaanisha kuwa kiini cha atomu yake huwa na protoni 99 na elektroni 99. Ni elementi sintetiki, maana haitokei kiasili, bali inategenezwa katika maabara. Sababu ni unururifu wake pamoja na nusumaisha ya siku 40 hadi 471 pekee. Isotopi zake zote ni nururifu, hazidumu.

Einsteini inang'aa kwa rangi ya buluu wakati wa giza kutokana na unururifu wake

Katika jedwali la elementi Einsteini huhesabiwa kati ya aktinidi ambako ina nafasi ya saba. Isotopi ya kudumu zaidi ya Einsteini ina protoni 99 na neutroni 153. Kuna isotopi 19 tofauti (zote nururifu).

Einsteini iligunduliwa mara ya kwanza mnamo 1952 na Albert Ghiorso na timu yake ya wanasayansi waliochungulia takataka iliyobaki baada ya mlipuko wa bomu ya hidrojeni ya kwanta, ikatambuliwa kama elementi katika Chuo Kikuu cha Kalifornia, Berkeley.

Jina lilichaguliwa kwa kumbukumbu ya mwanafizilia mashuhuri Albert Einstein.

Hakuna matumizi ya kweli yanayojulikana nje ya utafiti wa kisayansi.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Einsteini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.