Elbe ni mto mkubwa nchini Ujerumani na Ucheki.

Elbe
Elbe karibu na Děčín, Ucheki.
Chanzo Milima ya Krkonoše (Riesengebirge)
Mdomo Bahari ya Kaskazini
Nchi Ujerumani, Ucheki
Urefu 1,091 km
Kimo cha chanzo 1,386 m
Tawimito upande wa kulia Schwarze Elster, Havel, Löcknitz, Elde, Sude, Boize, Bille, Alster , Pinnau, Krückau, Stör
Tawimito upande wa kushoto Moldau, Eger, Mulde, Saale, Tanger, Aland, Jeetzel, Ilmenau, Este, Schwinge, Oste
Mkondo 711 m³/s
Eneo la beseni 148,268 km²
Miji mikubwa kando lake Dresden, Magdeburg, Hamburg
Kuanzia Hamburg hadi bahari ya Kaskazini mdomo wa Elbe huwa pana sana
Beseni ya mto Elbe

Inaanza kwa jina la Kicheki "labe" katika milima ya Krkonoše (Kijer.: Riesengebirge) karibu na mpaka wa kaskazini ya Ucheki.

Inapita sehemu kubwa ya Ujerumani wa Mashariki na Kaskazini na kuishia katika Bahari ya Kaskazini. Kuanzia mji wa Hamburg mwendo wa mto hupanuka sana maana maji ya bahari kupwa na kupwaa hucheza huingia hadi hapa.

Elbe ni njia muhimu ya meli za mtoni. Meli kubwa za bahari zinafika hadi bandari ya Hamburg kwa kutumia mdomo mpana wa Elbe.

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Elbe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.