Emmanuel Cosmas Msoka
Emmanuel Cosmas Msoka ni Mtanzania mwanaharakati na mbunifu mwenye kujitolea kwa haki za watoto na vijana, pamoja na kuwa chanzo cha mabadiliko. Wakati wa janga la COVID-19, Emmanuel aliweza kubuni mashine ya kunawa mikono ambayo iliongeza usafi kwa kuwa ni moja ya hatua muhimu za kuzuia dhidi ya ugonjwa hu. Kwa msaada wa shirika nchini Tanzania, ameweza kusambaza zaidi ya vituo vyingi mashine hizo za kunawa mikono 400 katika Kaskazini mwa Tanzania.[1]
Emmanuel Cosmas Msoka | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Emmanuel Cosmas Msoka |
Nchi | Tanzania |
Kazi yake | Mwanaharakati |
Ana uzoefu mkubwa katika kujitolea na mafunzo ya uongozi na ametoa muda mwingi kusaidia watoto na vijana wengine. Emmanuel alipendekezwa kwa Tuzo ya Kimataifa ya Amani ya Watoto, inayotolewa kila mwaka kwa mtoto ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa katika kutetea haki za watoto.
Emmanuel anaamini katika kuwawezesha watoto, elimu, ubunifu, na kama njia muhimu ya kukuza haki za watoto.
Amechaguliwa kama Msemaji wa Vijana wa UNICEF 2020 kwa masuala ya maji, usafi, na uvumbuzi. Juhudi zake zinaonyesha jinsi vijana wanaweza kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao na kuchangia katika maendeleo ya nchi yao.[2]
Tuzo
haririEmmanuel Msoka Kijana Mtanzania alishinda Tuzo ya Amani ya ( Davis) Nchini Marekani. amekuwa Balozi wa Vijana wa UNICEF, Tuzo hiyo inaambatana na ruzuku ambazo anatarajia kutumia kujenga maktaba ya amani kisiwani Zanzibar. Emmanuel amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya vijana ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya uongozi, ujasiriamali, ubunifu, na huduma za kijamii katika shule mbalimbali kaskazini mwa Tanzania. Emmanuel alitambuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa miongoni mwa mashujaa wa kuleta mabadiliko katika chapisho la “Unheard Pandemic Hero” lililochapishwa na shirika la watoto duniani, UNICEF.[3]
Emmanuel ambaye amekuwa ni mbunifu aliyeshinda tuzo mbali mbali za ubunifu ndani na nje ya Tanzania anatambuliwa pia kuwa kijana mwenye mchango mkubwa kwa jamii yake na umoja wa mataifa geneva, makao makuu ya Umoja wa mataifa marekani, UNICEF Tanzania, na UNICEF Canada.
Emmanuel anatarajia kujenga maktaba ndogo ya Amani Zanzibar akishirikiana na wadau mbalimbali na anaalika washirika na watu binafsi ambao watapenda kuchangia ujenzi wa maktaba hiyo ya amani. Katika vitu ambavyo mashirika yanaweza kuchangia ni pamoja na machapisho ya amani, vitabu, majarida na makala mbalimbali ambayo yanaweza kuwekwa kwenye maktaba hiyo.
Emmanuel pia anatambulika kwa hotuba yake ya amani aliyoitoa marekani mwaka jana katika wiki ya elimu, ananukuliwa akisema “Amani ndio mzizi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii, Na familia ndio nguzo ya jamii, Msingi wa familia ni Upendo, Mshikamano na Amani, Familia inapokuwa na Amani maendeleo katika jamii yataonekana.”
Hivi sasa Emmanuel anasomea uchumi na diplomasia ya kibiashara marekani, anatarajia kutumia elimu yake katika kuendeleza ukuaji wa uchumi nchini Tanzania na Afrika. Emmanuel amesema “huu ni mwanzo wa safari ndefu ya kidiplomasia na safari ya kuendeleza jamii yangu. Ninatarajia kufanya makubwa kwa kuanzia nyumbani Tanzania”.
Marejeo
hariri- ↑ "Emmanuel Cosmas Msoka - An Inspiring story of a young Innovator, Activist, and Changemaker". Voices of Youth (kwa Kiingereza). 2022-03-26. Iliwekwa mnamo 2024-05-05.
- ↑ "Activist Emmanuel Cosmas Msoka from Tanzania is leading by example". Voices of Youth (kwa Kiingereza). 2021-11-13. Iliwekwa mnamo 2024-05-05.
- ↑ "Mtanzania ashinda tuzo ya amani Marekani". TanzaniaWeb. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-05-05. Iliwekwa mnamo 2024-05-05.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Emmanuel Cosmas Msoka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |