Eneo la Ruweng ni eneo maalum la kiutawala nchini Sudan Kusini. [2] Eneo hilo lilijulikana kama Jimbo la Ruweng kati ya tarehe 2 Oktoba 2015 na 22 Februari 2020 wakati lilipokuwa na hadhi ya jimbo la Sudan Kusini.

Ruweng State
Mahali paRuweng State
Mahali paRuweng State
Mahali pa Ruweng katika Sudan Kusini
Bendera ya South Sudan South Sudan Sudan Kusini
Makao makuu Panrieng[1]
Idadi ya kaunti 8
Idadi ya manispaa
Serikali
 - Gavana Mayol Kur Akuei
Idadi ya wakazi (Kadirio la 2014)
 - Wakazi kwa ujumla 246,360

Ruweng ni eneo lenye mafuta ghafi.

Historia

hariri

Wakati wa uhuru wa Sudan Kusini, Ruweng ilikuwa sehemu ya Jimbo la Umoja. Tangu mwaka 2009 Wadinka, ambao ni wenyeji wa Ruweng, walilalamika kutopewa haki zao kutoka kwa Wanuer ambao ni wengi katika jimbo la Umoja[3]. Kutokana na malalamiko hayo Rais Salva Kiir alitoa amri ya kuanzisha majimbo 32 kwenye mwaka 2015 badala ya majimbo 10 yaliyotajwa na katiba. [4] Amri hiyo ilianzisha majimbo mapya pamoja na Ruweng kuwa jimbo.[5][6] Mayol Kur Akuei aliteuliwa kuwa Gavana mwaka wa 2015. [7]

Mwaka 2020 majimbo 10 ya awali yalirudishwa lakini Ruweng ilikuwa moja kati ya maeneo maalum matatu ya kiutawala yaliyopo moja kwa moja chini ya serikali kuu.

Wakuu wa eneo

hariri
Kipindi Jina Chama
Mei 2015 - 2017 Mayol Kur Akuei SPLM
2017-2017 Theji Da Aduot Deng SPLM(IO)
2017 - Juni 2020 Wao ni Michar Kuol SPLM(IO)
2019-2020 Dkt.Lawrence Miabok Wuor Piok SPLM]]
Juni 2020 - 2021 William Chol Awanlith SPLM
Juni 2021 - Mei 2022 Mhe. Peter Daau Chopkuer SPLM
Mei 2022 - Juni 2022 Mhe. Tiop Manyluak Diraan SPLM
Juni 2022–Sasa Stephano Wieu Mialek SPLM [8]

Jiografia

hariri

Eneo la Kiutawala la Ruweng liko katika sehemu ya kaskazini ya Sudan Kusini na makao yake makuu yako Pariang. Inapakana na Jimbo la zamani la Fashoda upande wa mashariki na Jimbo la Fangak upande wa kusini-mashariki, Jimbo la Liech Kaskazini upande wa kusini, Jimbo la Twic upande wa kusini-magharibi, Abyei upande wa magharibi, na Sudan upande wa kaskazini.

Uchumi

hariri

Ni eneo linalozalisha mafuta kuliko maeneo yote mengine ya Sudan Kusini, kwa jumla karibu 80% ya mafuta ya Sudan Kusini yanazalishwa hapa, haswa katika uwanja wa mafuta wa Unity / Darbim (katika sehemu ya kusini), uwanja wa mafuta wa Heglig / Panthou (katika sehemu ya kaskazini-magharibi), uwanja wa mafuta cha Tomasouth/Kaloj (katika sehemu ya magharibi) na eneo la mafuta la Toor/Athony au maeneo mengine ya mafuta kama vile Labob/Miading na Munga/Wanhe Danluel na Maan Awal na maeneo mengine.

Ruweng kuna wanyama wengi na pia samaki. Kuna maziwa mawili ambayo ni Ziwa Jau (katika sehemu ya kaskazini) na Ziwa No (katika sehemu ya kusini), ambapo Mto Bahr el Ghazal unaishia na kujiunga na Nile Nyeupe.

Wakazi

hariri

Wakazi wengi ni Wadinka wa Ruweng ambao ni Wadinka wa Panaruu wenye makabila madogo 12 na Wadinka wa Aloor au Ruweng Biemnom wenye makabila madogo 6.

Mgawanyiko wa kiutawala

hariri

Eneo hilo lina wilaya 2 (counties): Panriang na Abiemnom .

Marejeo

hariri
  1. "What exactly is Riek Machar is planning to achieve". Wël Yam. 1 Agosti 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-21. Iliwekwa mnamo 14 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "After 6 years of war, will peace finally come to South Sudan?".
  3. https://radiotamazuj.org/en/news/article/opinion-ruweng-has-had-clear-administrative-boundaries-since-1905 Ilihifadhiwa 19 Machi 2023 kwenye Wayback Machine. Opinion | Ruweng has had clear administrative boundaries since 1905, tovuti ya radiotamazuj.org, 24 Februari 2020
  4. "Kiir and Makuei want 28 states in South Sudan". Retrieved on 2023-03-19. Archived from the original on 2015-12-08. 
  5. "Kiir pressured into taking decree to parliament for approval". Retrieved on 2023-03-19. Archived from the original on 2016-03-04. 
  6. "South Sudan's Kiir appoints governors of 28 new states". 
  7. "South Sudan's President appoints 28 Governors, defies peace agreement". Retrieved on 2023-03-19. Archived from the original on 2016-02-02. 
  8. "South Sudan's Kiir sacks Ruweng chief administrator". Juni 6, 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-09. Iliwekwa mnamo 2023-03-19.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Eneo la Ruweng kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.