Epimako wa Pelusi (223 hivi - 250 hivi) alikuwa kijana Mkristo wa mji huo wa Misri ambaye wakati wa dhuluma ya kaisari Decius alijitosa kupindua altari ya Kipagani ambapo Wakristo walikuwa wanalazimishwa kutoa sadaka kinyume cha imani yao.

Kwa hiyo aliteswa na kukatwa kichwa huko Aleksandria.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Oktoba[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.