Fungo-bukini

(Elekezwa kutoka Euplerinae)
Fungo-bukini
Fosa (Cryptoprocta ferox)
Fosa (Cryptoprocta ferox)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: [Chordata]] (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbuai)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Eupleridae (Wanyama walio na mnasaba na fungo-bukini)
Nusufamilia: Euplerinae (Wanyama wanaofanana na fungo-bukini)
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 4:

Fungo-bukini ni wanyama wadogo hadi wakubwa kiasi wa Madagaska wanaoainishwa katika nusufamilia Euplerinae wa familia Eupleridae na ambao wanafanana na fungo wa bara la Afrika. Pamoja na nguchiro-bukini (nusufamilia Galidiinae) wana mhenga mmoja aliyekuwa aina ya nguchiro na aliyevuka Mlango wa Msumbiji miaka milioni 20 iliyopita.

Wanyama hawa ni kama fungo wadogo au nguchiro, isipokuwa fosa. Mdogo kuliko wote ni fungo-bukini miraba (sm 20 na g 1500-2000) na mkubwa ni fosa (sm 70-80 na kg 5.5-8.6). Rangi yao ni kahawia au kahawianyekundu.

Wanatokea misituni na hula vertebrata kama lemuri, tandaraka, wagugunaji, mijusi na ndege (fosa na fungo-bukini miraba) au invertebrata kama nyungunyungu, konokono, konokono uchi na lava (falanuki).

Spishi

hariri