Eva Lucia Saulitis (alizaliwa 10 Mei 1963 -amefariki 16 Januari 2016) alikuwa mwanabiolojia wa bahari na mwandishi wa mashairi wa Marekani, akiishi Alaska.

Maisha na Elimu ya Awali

hariri

Saulitis alizaliwa Bronx na kuishi Silver Creek, New York,[1] akiwa ni binti wa wahamiaji kutoka Latvia, Janis (John) Saulitis na Asja Ivins Saulitis.[2]

Saulitis alisoma makundi ya aina ya nyangumi wa aina ya orca katika chuo cha Prince William Sound.[3][4] Saulitis alifundisha uandishi wa ubunifu katika Chuo cha Kenai Peninsula , na katika programu ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Alaska Anchorage.[5] Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Mkutano wa Waandishi wa Kachemak Bay, na mwanzilishi mwenza wa North Gulf Oceanic Society.[6]

Maisha ya kibinafsi na urithi

hariri

Saulitis na mumewe,ambaye ni mtafiti wa biolojia Craig Matkin, walikuwa na nyumba huko Alaska na Hawaii.[7][8]Saulitis Alifariki mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 52 kutokana na saratani ya matiti, nyumbani kwake Homer, Alaska.

Marejeo

hariri
  1. Saulitis, Eva (2017). "Katika Mwili Ambao Zamani Ulinitolea". The Sun Magazine (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-09.
  2. "Tangazo la Kifo la Eva Lucia Saulitis". Chautauqua Today. Januari 24, 2016. Iliwekwa mnamo 2022-07-09.
  3. "Eva Saulitis". Orion Magazine (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-09.
  4. Genoways, Ted (Januari 20, 2016). "Mwanamke Anayependa Orcas". NRDC (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-09.
  5. "Eva Saulitis". Alaska Arts and Culture Foundation. Iliwekwa mnamo 2022-07-09.
  6. "Eva Saulitis". Poetry Foundation (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-09.
  7. Saulitis, Eva (Agosti 2015). "When No One Is Watching". The Sun Magazine (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-09.
  8. "Two Alaska Authors Share Secrets of the Craft", The Honolulu Advertiser, 2008-01-08, pp. 35. 
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eva Saulitis kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.