Félix Tshisekedi
Félix Antoine Tshisekedi (alizaliwa 13 Juni 1963) ni kiongozi wa chama cha Muungano wa Demokrasia na Maendeleo ya Jamii (UDPS), chama cha zamani na chama cha upinzani cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mwishoni mwa mwaka 2008, Tshisekedi alitajwa kuwa Katibu Mkuu wa UDPS wa mahusiano ya nje. Mnamo Novemba 2011, alipata kiti katika Bunge la Taifa, akiwakilisha mji wa Mbuji Mayi katika mkoa wa Kasai-Mashariki.
Tarehe 10 Januari 2019, ilitangazwa kwamba Tshisekedi amechaguliwa kuwa rais wa nchi katika uchaguzi mkuu wa tarehe 30 Desemba 2018, kwa kuwashinda Martin Fayulu na Emmanuel Ramazani Shadary.
Baada ya Fayulu kukata rufaa, tarehe 19 Januari Mahakama Kuu ilithibisha ushindi wa Tshisekedi, ingawa Umoja wa Afrika, Kanisa Katoliki na nchi kama Ufaransa wa Ubelgiji walipinga tena.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Félix Tshisekedi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |