Uyabisi wa Misuli
Uyabisi wa Misuli (Fibromyalgia, FM) ni ugonjwa wenye dalili za maumivu ya muda mrefu yaliyoenea kote mwilini na mwitikio wa maumivu makali kwa shinikizo yoyote kwenye mwili.[2] Dalili nyingine ni pamoja na uchovu mwingi kiasi kwamba shughuli za kawaida huathiriwa, matatizo ya usingizi na matatizo ya kumbukumbu.[3] Baadhi ya watu pia huripoti dalili za miguu kutotulia, matatizo ya utumbo au kibofu cha mkojo kuwasha, kufa ganzi na kuhisi mwasho na kuwa na hisia kali kwa kelele, mwanga au halijoto.[4] Mara nyingi huhusishwa na unyogovu, wasiwasi na ugonjwa wa kiakili unaotokana na kiwewe.[3] Aina nyingine za maumivu ya muda mrefu pia hutokea mara kwa mara.[3]
Uyabisi wa Misuli | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Matamshi | |
Kundi Maalumu | Matibabu ya Akili, magonjwa ya yabisi baridi, neurolojia |
Dalili | Maumivu yaliyoenea, hisia ya uchovu, matatizo ya usingizi[2][3] |
Muda wa kawaida wa kuanza kwake | Watu wenye umri wa kati[4] |
Muda | Ya muda mrefu[2] |
Visababishi | Hakijulikani[3][4] |
Njia ya kuitambua hali hii | Kulingana na dalili zilizopo baada ya kuondoa sababu zingine zinazoweza kuusababisha[3][4] |
Utambuzi tofauti | Ugonjwa wa Polymyalgia rheumatica, ugonjwa wa yabisi-baridi (rheumatoid arthritis), ugonjwa wa yabisi-barid (osteoarthritis), ugonjwa wa dundumio (thyroid)[5] |
Matibabu | Kulala na mazoezi ya kutosha, lishe bora[4] |
Dawa | Duloxetine, milnacipran, pregabalin, gabapentin[4][6] |
Utabiri wa kutokea kwake | Umri wa kuishi wa kawaida[4] |
Idadi ya utokeaji wake | asilimia 2–8%[3] |
Kisababishi hakijulikani, hata hivyo, inaaminika kuwa inahusisha mchanganyiko wa mambo ya kijenetikia na ya mazingira.[3][4] Hali hiyo hutokea katika familia na jeni nyingi zinaaminika kuhusika.[7] Sababu za kimazingira zinaweza kujumuisha mfadhaiko wa kisaikolojia, kiwewe na maambukizi fulani.[3] Maumivu yanaonekana kuwa yanatokana na michakato katika mfumo mkuu wa neva na hali hiyo inajulikana kama "ugonjwa wa kihisia wa neva ya kati".[2][3] Fibromyalgia inatambuliwa kama ugonjwa na Taasisi za Kitaifa za Afya za Marekani na Chuo cha Marekani cha Rheumatology .[4][8] Hakuna vipimo maalum wa utambuzi wa ugonjwa.[4] Utambuzi wa ugonjwa unahusisha kwanza kuondoa sababu zingine zinazoweza kuusababisha na kuthibitisha kuwa kuna idadi fulani ya dalili.[3][4]
Matibabu ya Fibromyalgia yanaweza kuwa magumu.[4] Mapendekezo ya matibabu mara nyingi hujumuisha maelekezo ya kulala vya kutosha, kufanya mazoezi mara kwa mara, na kula vyakula vyenye lishe bora.[4] Tiba ya kitabia ya utambuzi (CBT) inaweza pia kusaidia.[3][9] Dawa za duloxetine, milnacipran au pregabalin zinaweza kutumiwa.[4] Matumizi ya dawa za maumivu ya opioidi ni ya utata, huku wengine wakisema manufaa yana ushahidi hafifu wa kuunga mkono utumiaji wake[4][10] na wengine wakisema kwamba utumiaji wa opioid kidogo inaweza kuwa sawa ikiwa dawa zingine hazifanyi kazi.[11] Virutubisho vya lishe havina ushahidi wa kuunga mkono matumizi yao.[4] Ingawa fibromyalgia inaweza kudumu kwa muda mrefu, haisababishi kifo au uharibifu wa tishu za mwili.[4]
Fibromyalgia inakadiriwa kuwa inaathiri asilimia 2 hadi 8 ya idadi ya watu.[3] Wanawake huathiriwa mara mbili zaidi kuliko wanaume.[3] Viwango vinaonekana sawa katika maeneo tofauti ya ulimwengu na kati ya tamaduni tofauti.[3] Fibromyalgia ilifafanuliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1990 na vigezo vikasasishwa mwaka wa 2011.[3] Kuna utata kuhusu uainishaji, utambuzi na matibabu ya fibromyalgia.[12][13] Ingawa wengine wanahisi kuwa utambuzi wa fibromyalgia unaweza kuathiri mtu vibaya, utafiti mwingine umebaini kuwa unaweza ukawa na manufaa.[3] Neno "fibromyalgia" linatokana na neno la lugha ya New Latin fibro-, ikimaanisha "tishu zenye nyuzi", Kigiriki μυώ myo-, "misuli", na Kigiriki άλγος algos, "maumivu"; kwa hivyo, tafsiri ya moja kwa moja ya neno hilo inamaanisha "maumivu ya tishu za kuunganisha zenye nyuzi na misuli".[14]
Marejeo
hariri- ↑ "fibromyalgia". Collins Dictionaries. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Oktoba 2015. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2016.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 Ngian GS, Guymer EK, Littlejohn GO (Februari 2011). "The use of opioids in fibromyalgia". Int J Rheum Dis. 14 (1): 6–11. doi:10.1111/j.1756-185X.2010.01567.x. PMID 21303476.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 3.11 3.12 3.13 3.14 3.15 3.16 Clauw, Daniel J. (16 Aprili 2014). "Fibromyalgia". JAMA. 311 (15): 1547–55. doi:10.1001/jama.2014.3266. PMID 24737367.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.00 4.01 4.02 4.03 4.04 4.05 4.06 4.07 4.08 4.09 4.10 4.11 4.12 4.13 4.14 4.15 4.16 "Questions and Answers about Fibromyalgia". NIAMS. Julai 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 15 Machi 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ferri, Fred F. (2010). Ferri's differential diagnosis : a practical guide to the differential diagnosis of symptoms, signs, and clinical disorders (tol. la 2nd). Philadelphia, PA: Elsevier/Mosby. uk. Chapter F. ISBN 978-0323076999.
- ↑ Cooper, TE; Derry, S; Wiffen, PJ; Moore, RA (3 Januari 2017). "Gabapentin for fibromyalgia pain in adults". The Cochrane Database of Systematic Reviews. 1: CD012188. doi:10.1002/14651858.CD012188.pub2. PMC 6465053. PMID 28045473.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Buskila D, Sarzi-Puttini P (2006). "Biology and therapy of fibromyalgia. Genetic aspects of fibromyalgia syndrome". Arthritis Research & Therapy. 8 (5): 218. doi:10.1186/ar2005. PMC 1779444. PMID 16887010.
{{cite journal}}
: CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ "Fibromyalgia". American College of Rheumatology. Mei 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Mascarenhas, Rodrigo Oliveira; Souza, Mateus Bastos; Oliveira, Murilo Xavier; Lacerda, Ana Cristina; Mendonça, Vanessa Amaral; Henschke, Nicholas; Oliveira, Vinícius Cunha (26 Oktoba 2020). "Association of Therapies With Reduced Pain and Improved Quality of Life in Patients With Fibromyalgia: A Systematic Review and Meta-analysis". JAMA Internal Medicine. doi:10.1001/jamainternmed.2020.5651.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Goldenberg, DL; Clauw, DJ; Palmer, RE; Clair, AG (Mei 2016). "Opioid Use in Fibromyalgia: A Cautionary Tale". Mayo Clinic Proceedings (Review). 91 (5): 640–8. doi:10.1016/j.mayocp.2016.02.002. PMID 26975749. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 22 Julai 2020.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Sumpton, JE; Moulin, DE (2014). Fibromyalgia. Juz. la 119. ku. 513–27. doi:10.1016/B978-0-7020-4086-3.00033-3. ISBN 9780702040863. PMID 24365316.
{{cite book}}
:|work=
ignored (help) - ↑ Häuser W, Eich W, Herrmann M, Nutzinger DO, Schiltenwolf M, Henningsen P (Juni 2009). "Fibromyalgia syndrome: classification, diagnosis, and treatment". Dtsch Arztebl Int. 106 (23): 383–91. doi:10.3238/arztebl.2009.0383. PMC 2712241. PMID 19623319.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Wang, SM; Han, C; Lee, SJ; Patkar, AA; Masand, PS; Pae, CU (Juni 2015). "Fibromyalgia diagnosis: a review of the past, present and future". Expert Review of Neurotherapeutics. 15 (6): 667–79. doi:10.1586/14737175.2015.1046841. PMID 26035624.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Bergmann, Uri (2012). Neurobiological foundations for EMDR practice. New York, NY: Springer Pub. Co. uk. 165. ISBN 9780826109385.