Flora na Maria (walifariki Cordoba, leo nchini Hispania, 851) walikuwa Wakristo waliofia imani yao chini ya utawala wa Waislamu.

Picha ya Mt. Flora katika kanisa kuu la Cordoba.

Flora alikuwa na baba Mwislamu na mama Mkristo, kumbe Maria kinyume chake alikuwa na baba Mkristo na mama Mwislamu, ila alibatizwa muda mfupi baada ya kuolewa. Walipokutana waliamua kujitosa kupinga Uislamu hadharani hata wakakatwa kichwa[1][2][3].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu mabikira wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 24 Novemba [4][5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.