Kadhi (kutoka Kiarabu: القاضي, al-qadi) ni cheo cha jaji kwenye mahakama ya Kiislamu anayetumia kanuni za shari'a kufikia hukumu zake.

Kesi iliyojadiliwa mbele ya kadhi: nakhshi ya karne ya 14.

Katika jumuiya ya Kiislamu ya zamani kadhi aliangalia masuala yote ya haki. Siku hizi karibu nchi zote zinatumia pia sheria zinazotofautiana katika kesi za madai, za adhabu na za jinai. Hata hivyo, katika nchi za Kiarabu majaji wanaendelea kuitwa kadhi hata wakitumia sheria iliyotungwa bungeni.

Katika nchi kadhaa kuna utaratibu kwamba kesi za binafsi za Waislamu (kama vile urithi, ndoa, talaka) zinaamuliwa na mahakama ya kadhi iliyopo kando ya mahakama za kawaida, mifano yake ni Kenya na Zanzibar.

Kwa desturi kadhi ni mtu mzima, mwanamume, mwenye akili timamu anayejulikana ana kiwango cha elimu ya shari'a. Kwa kawaida aliamua peke yake, na hapakuwa na rufaa dhidi ya hukumu[1]

Wasomi Waislamu wanatofautiana kama wanawake wanafaa kuwa kadhi[2]. Hata hivyo, idadi ya wanawake katika nafasi ya kadhi imeongezeka: Malaysia imeanza mwaka 2010 kupeleka wanawake katika nafasi hiyo, nchi nyingine kama Indonesia, Pakistan na Sudan zimefuata.[3]

Marejeo hariri

  1. Qadi, tovuti ya Britannica, iliangaliwa Desemba 2019
  2. Ruling on appointment of women as a judge, Fatwa ya kukataa kadhi wa kike kwenye tovuti islanqa.info, iliyotolewa na shehe wa Saudia
  3. The female face of Islamic law in Malaysia, tovuti ya aljazeera.com ya 16 Aug 2017
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.