Fonetiki (kutoka Kiingereza "Phonetics") ni tawi la sayansi ya isimu. Inashughulikia uchunguzi wa sauti za lugha za binadamu, pamoja na utamkaji na usikiaji wake. Kwa ujumla, fonetiki ni tawi la isimu linalochunguza jinsi sauti zinavyozalishwa, zinavyosafirishwa na zinavyomfikia msikilizaji.

Etimolojia ya neno fonetiki imebeba dhana mbili: foni na etiki. Foni humaanisha sauti, ilihali etiki ni dhana pana kidogo.

Vitamkwa huandikwa kwa kutumia alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa (au kifupi cha jina lake kwa Kiingereza, International Phonetic Alphabet).

Fonetiki inagawanyika katika:

  • fonetiki akustika
  • fonetiki maabara (au fonetiki majaribio)
  • fonetiki masikizi
  • fonetiki matamshi
  • fonetiki tibamatamshi

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Ya Kiswahili hariri

  • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mengineyo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fonetiki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.