Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa

Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa (kwa Kiingereza: International Phonetic Alphabet, kifupi IPA) ni mfumo wa alfabeti unaolenga kuonyesha sauti za lugha zote duniani. Imetungwa na wataalamu wa isimu wanaoshirikiana katika Shirika la Kimataifa la Fonetiki (International Phonetic Association). Inatumiwa na watunga kamusi, walimu na wanafunzi wa lugha za kigeni, wanaisimu na wafasiri kote duniani. Kwa hiyo tunakuta alama zake katika kamusi na mara nyingi pia kwenye makala za Wikipedia.

Msingi wa IPA ni alfabeti ya Kilatini pamoja na herufi za pekee zilizochukuliwa kutoka alfabeti nyingine. Herufi hizo zinaunganishwa na alama za pekee.

Mfano ni alama zinazoonyesha sauti tofauti ambazo mara nyingi zinaonyeshwa kwa herufi "A" ambazo zinaweza kuwa na sauti tofauti katika lugha na lahaja mbalimbali kama vile a   ? , ɐ   ?, ɑ   ?, ɒ   ?, æ   ?, ɑ̃ au ʌ   ? (bofya pembetatu ndogo kwa kusikia sauti).

Orodha ya alama zote za IPA pamoja na sauti inapatikana katika Wikipedia ya Kijerumani hapa de:Liste_der_IPA-Zeichen

Tangu masahihisho ya mwaka 2005[1] kuna herufi 107 na alama za pekee 56.

Tanbihi hariri

  1. "IPA: Alphabet". Langsci.ucl.ac.uk. Archived from the original on 10 October 2012. Retrieved 20 November 2012.
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.