Huzuni (kutoka neno la Kiarabu) ni hali ya simanzi inayompata mtu au mnyama kwa kufikiwa na jambo lisilomfurahisha. Ni kati ya maono ya msingi. Huzuni hupelekea mtu kujihisi mpweke na kukosa tumaini.

Sehemu ya sanamu ya mwaka 1672 kuhusu Kuzikwa kwa Kristo, ikimuonyesha Maria Magdalena akitokwa na machozi kwa huzuni.

Kadiri ya silika, baadhi wanaelekea huzuni kuliko kawaida.