G.W.M
Gangstas With Matatizo (mara nyingi hufupishwa kwa: G.W.M) lilikuwa kundi la muziki wa hip hop lililotamba sana katika miaka ya tisini huko nchini Tanzania. Kundi linaundwa na KR (jina halisi Rashid Ziada) na D-Chief (jina halisi Robert E. Makala) na Easy Dope (jina halisi Richard Makala) kaka mkubwa wa D Chief. Kundi lilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1997.
G.W.M | |
---|---|
D-Chief na KR | |
Taarifa za awali | |
Chimbuko | Dar es Salaam Tanzania |
Miaka ya kazi | 1997– |
Studio | Don Bosco |
Ameshirikiana na | Mr. II |
Wanachama wa zamani | |
KR D-Chief Easy Dope |
Hata hivyo, ndugu hao kina Makala walianza kurap tangu mwaka 1993 wakati bado wapo shule. Baba yao alikuwa fundi/mkali wa muziki wa asili nchini Tanzania. K.R. aliungana nao mnamo mwaka wa 1995. Katika mwaka huo walishinda katika mashindano ya kutafuta wasanii wenye vipaji lililoandaliwa na Don Bosco, mmiliki mmoja wa studio huko mjini Dar es Salaam. Jambo hili liliwapatia fursa ya kuweza kurekodi baadhi ya nyimbo zao zilizosaidiwa na baadhi ya mabendi maarufu kwa kipindi hicho. Nyimbo zao zikawa maarufu mno.
GWM walipata kutumbuiza katika matamasha ya kulipwa kwa zaidi ya mara 20 katika kipindi cha mwaka wa 1997, ambapo jambo hili lilikuwa rekodi nzuri hasa kwa kufuatia kilikuwa kikundi cha rap kwa Dar. Mashabiki wao wengi walikuwa wanafunzi wa sekondari, wanafunzi wa vyuo vya kawaida na vyuo vikuu. Hili pia huenda sawa kwa makundi mengine ya rap ya Dar kwa kipindi hiko. Wimbo wao wa Yemenikuta ulikuwa moja kati ya nyimbo kali sana zilizobamba katika mwemzi wa Novemba, 1997. Wimbo ulihusu harakati za maisha ya kila siku wanayokutana nayo katika mitaa ya Dar.
Kwa upande wa GWM, wao walikomaa zaidi katika kuimba rap halisi kwa Kiswahili tu. Wanapamba na hali ngumu ya maisha ya mjini Dar es Salaam, inabidi uwe mjanja ndo utoke jijini humo. Lilikuwa moja kati ya makundi yaliyokuwa yanaheshimika kwa vijana wapya kutoka shule kwa miaka hiyo ya 1997. Walifahamika muda mfupi kwa mashairi yao ya kijanja nchini Tanzania. Mara ya kwanza kuona mwangaza wa redio ilikuwa kwa kibao chao cha 'Cheza Mbali na Kasheshe' na nyimbo zao nyinginezo zilizosheheni mistari ya maneno ya mjini kwa kipindi hiko.
Albamu yao ya kwanza ingelitoka katika miaka hiyohiyo, lakini kwa vile mpango ulienda kusi matokeo yake ikaja kutolewa mnamo mwaka wa 2000 pekee, muda kiasi tangu kuvuma. Mwaka huohuo wa 2000, KR akajiunga na Wachuja Nafaka.[1]
Diskografia
haririKatika harakati za muziki G.W.M wamepata kutoa albamu moja tu mnamo mwaka wa 2000. Albamu iliitwa:
- Mikosi - 2000
Baadhi ya nyimbo zao maarufu
hariri- Cheza Mbali na Kasheshe (1995)
- Yamenikuta - wakiwa na Mr. II (1997)
- Kipe Kitu (1998)
- Kamua wakiwa na Juma Nature (2003)
Tazama pia
haririMarejeo
haririViungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu G.W.M kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |