Juma Nature
mwanamuziki wa Tanzania
Juma Kassim Ally, anayejulikana zaidi kama Juma Nature au Sir Nature (alizaliwa Dar es Salaam mwaka 1980), ni mwanamuziki wa aina ya Bongo Flava na Hip Hop kutoka Tanzania. Ni mwanzilishi wa kundi maarufu la TMK Wanaume Family.
Juma Nature | |
---|---|
Juma Nature
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Juma Kassim Ally |
Pia anajulikana kama | Sir. Nature Kibla Msitu wa Vina Jitu la Maneno ya Shombo |
Amezaliwa | 1980 |
Kazi yake | Rapa |
Miaka ya kazi | 1997 - hadi leo |
Studio | Bongo Records Sound Crafters Records Mj Records |
Ame/Wameshirikiana na | Dknob Mh Temba Dark Master TID Solo Thang Professor Jay AY Inspector Haroun Chegge Mandojo na Domokaya Zay B. |
Juma Nature ni msanii mbunifu ambaye si mtunzi wa mashairi tu, bali pia ana kipaji cha kipekee kinachochangiwa na sauti yake nzuri ya uimbaji. Moja ya sababu zinazoufanya muziki wake kupendwa sana Afrika Mashariki ni mashairi yake yenye maana na ujumbe wa kina. Miongoni mwa nyimbo zake zilizompa heshima kubwa kitaifa ni Umoja wa Tanzania, wimbo uliolenga kupatanisha mgogoro wa kisiasa kati ya vyama vya CCM na CUF. Mbali na wimbo huo, Nature ametoa nyimbo nyingi zenye mafunzo na ujumbe wa kizalendo kwa Taifa. [1][2]
Albamu alizotoa
haririMarejeo
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Juma Nature kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |