Georg Simon Ohm
Georg Simon Ohm (Erlangen, 16 Machi 1789 - 6 Julai 1854) alikuwa mwanafizikia wa Ujerumani na mtaalamu wa hisabati.
Georg alizaliwa katika familia ya Waprotestanti. Kama mwalimu wa shule, Ohm alichungulia hasa elimu mpya ya umeme akifuatilia mambo mapya yaliyopatikana tangu ugunduzi wa seli ya kielektrokemia na Mwitalia Alessandro Volta.
Kwa kutumia vifaa alivyovitengeneza mwenyewe, Ohm aligundua kwamba kuna uwiano wa moja kwa moja kati ya ampea za mkondo wa umeme unaopita kwenye chombo na volti. Uhusiano huo unajulikana kama Kanuni ya Ohm (Ohm's law). Kizio cha kupimia ukinzani kimeitwa "Ohm" kwa heshima yake.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Georg Simon Ohm kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |