Fuko (Bathyergidae)
Fuko | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Fuko wa Damaraland (Fukomys damarensis)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 6: |
Mafuko hawa ni wanyama wa familia Bathyergidae ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama wengine waitwao fuko ni wanafamilia wa Chrysochloridae (oda Afrosoricida), Spalacidae (Rodentia), Talpidae (Soricomorpha) na Notoryctidae (Notoryctemorphia). Spishi zote za Bathyergidae zinatokea Afrika kusini kwa Sahara. Hula mizizi, matunguu na viazi. Kwa hivyo wanyama hawa wana meno manne makubwa mbele mdomoni. Huyatumia meno haya pia kwa kuchimba mahandaki yao. Macho na masikio yao ni madogo na mkia vilevile. Wamepoteza nusra uwezo wa kuona, lakini angalau spishi mbili wanaweza kuhisi nuru. Manyoya yao ni kama bahameli na yana rangi ya kahawia au hudhurungi, lakini fuko uchi hana manyoya. Takriban spishi zote huishi peke yao lakini fuko uchi na fuko wa Damaraland ni mamalia wa pekee ambao huishi kwa jamii za aina ya eusocial kama nyuki au mchwa. Jike mmoja na dume mmoja tu huzaa; wanyama wengine wa jamii ni gumba na husaidia kwa kutafuta chakula na kutunza makinda.
Spishi
hariri- Bathyergus janetta, Fuko-mchanga wa Namakwa (Namaqua Dune Mole Rat)
- Bathyergus suillus, Fuko-mchanga Kusi (Cape Dune Mole Rat)
- Cryptomys anomalus, Fuko wa Pretoria
- Cryptomys holosericeus, Fuko Manyoya-laini
- Cryptomys hottentotus, Fuko wa Kawaida (Common Mole Rat)
- Cryptomys natalensis, Fuko wa Natal
- Cryptomys nimrodi, Fuko wa Matabeleland (Matabeleland Mole Rat)
- Fukomys amatus, Fuko wa Zambia (Zambian Blesmol)
- Fukomys anselli, Fuko wa Ansell (Ansell's Blesmol)
- Fukomys bocagei, Fuko wa Bocage (Bocage's Blesmol)
- Fukomys damarensis, Fuko wa Damaraland (Damaraland Blesmol)
- Fukomys darlingi, Fuko wa Mashona (Mashona Blesmol)
- Fukomys foxi, Fuko wa Nijeria (Nigerian Blesmol)
- Fukomys ilariae[1], Fuko Somali (Somali striped Mole Rat)
- Fukomys kafuensis, Fuko wa Kafue (Kafue Blesmol)
- Fukomys mechowii, Fuko wa Mechow (Mechow's Blesmol)
- Fukomys micklemi, Fuko wa Kataba (Kataba Blesmol)
- Fukomys occlusus, Fuko wa Kigogo
- Fukomys ochraceocinereus, Fuko Ukaria (Ochre Blesmol)
- Fukomys vandewoestijneae, Fuko wa Caroline (Caroline's Blesmol)
- Fukomys whytei, Fuko wa Malawi (Malawian Blesmol)
- Fukomys zechi, Fuko wa Ghana (Ghana Blesmol)
- Georychus capensis, Fuko Kusi (Cape Blesmol)
- Heliophobius argenteocinereus, Fuko Fedha (Silvery Blesmol)
- Heterocephalus glaber, Fuko Uchi (Naked Mole Rat)
Picha
hariri-
Fuko-mchanga kusi
-
Fuko wa Ansell
-
Fuko wa Mechow
-
Fuko kusi
-
Fuko fedha
-
Fuko uchi
Marejeo
hariri- ↑ Gippoliti, S. & Amori, G. (2011). "A new species of mole-rat (Rodentia, Bathyergidae) from the Horn of Africa" (PDF). Zootaxa. 2918: 39–46.
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)