Giacomo Tedesco (amezaliwa Palermo, 1 Februari 1976) alikuwa mchezaji wa kandanda wa Italia ambaye alicheza kama kiungo katika ligi za Italia. Kwa sasa ni kocha.

Giacomo Tedesco
Tedesco(kulia)
Maelezo binafsi
Jina kamili Giacomo Tedesco
Tarehe ya kuzaliwa 1 Februari 1976
Mahala pa kuzaliwa    Palermo, Italia
Urefu 1.75m
Nafasi anayochezea Mchezaji wa kati
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Reggina
Namba 19
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
1994-1997
1997-2002
2000-2001
2003
2003-2007
2007-2009
2009
2010-2013
Palermo FC
Salernitana
→ Napoli (mpango wa mkopo)
Cosenza
Reggina
Catania
Bologna FC
[Reggina

* Magoli alioshinda

Tedesco akisherehekea kufungwa kwa bao dhidi ya timu pinzani.

Wasifu wa klabu hariri

Giacomo Tedesco alianza kucheza katika klabu yake ya nyumbani ya Palermo FC katika mwaka wa 1994. Alicheza katika mji wa Palermo kwa misimu mitatu akicheza katika mechi takriban 70 na kufunga mabao matatu. Katika mwaka wa 1997, alihamia klabu ya Salernitana, alipoenda na kucheza katika mechi 133 na kufunga mabao 13 kati ya miaka ya 1997 na 2007. Alihamia klabu ya Napoli katika msimu wa 200-2001. Katika miezi sita na klabu hiyo ya kusini mwa Uitalia,alicheza katika mechi 14. Katika mwaka wa 2003, yeye alihamia kwa muda mfupi klabu ya Cosenza ambapo yeye alifunga bao moja katika mechi 14. Baadaye katika mwaka wa 2003, alitia saini mkataba na klabu ya Reggina Calcio,alikocheza kwa miaka minne katika Ligi Kuu ya Uitalia. Alicheza zaidi ya mechi 120 katika klabu ya Reggina huku akifunga mabao 5. Katika mwaka wa 2007, licha ya kuwa na mafanikio katika mji wa Calabria, Tedesco alihamia klabu ya Kisicilia ya Calcio Catania. Tangu kujiunga na Catania, yeye alicheza katika mechi 50 na kufunga mabao manne katika misimu miwili. Alipokuwa na makocha , Walter Zenga na Silvio Baldini Tedesco, alikuwa akicheza mara kwa mara na alikuwa mchezaji wa bidii sana katika upande wa kushoto wa uwanja. Tarehe 9 Julai 2009, huduma za Tedesco ziliuziwa klabu ya Bologna FC iliyokuwa na mkataba na Tedesco wa urefu wa miaka miwili. Mnamo tarehe 14 Januari 2010, Tedesco alirudi Reggina kwa mpango uliopea Bologna Antonio Busce.

Binafsi hariri

Kaka yake, Giovanni Tedesco alicheza naye katika timu moja katika msimu wa 1997-98 katika klabu ya Salernitana.

Viungo vya nje hariri