Yosefu Maria Gambaro

(Elekezwa kutoka Giuseppe Maria Gambero)

Giuseppe Maria Gambaro (Galliate, Italia, 7 Agosti 1869 - 7 Julai 1900) alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo aliyefia imani huko China, alipokuwa mmisionari, akiuawa kwa kupigwa mawe huku akijitokeza pamoja na askofu Antonino Fantosati kutetea waumini wakati wa Uasi wa Waboksa [1].

Picha yake halisi.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 119.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila mwaka tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 7 Julai[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91736
  2. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.