Atukuzwe Baba
Atukuzwe Baba (kwa Kilatini Gloria Patri) ndiyo doksolojia (kutoka neno la Kigiriki: δοξολογία, linaloundwa na δόξα, doxa, "utukufu" na λογία, -logia, "neno")[1] inayotumika zaidi katika madhehebu mengi ya Ukristo.
Doksolojia ni shangilio fupi la kumsifu Mungu katika Ukristo, ambalo mara nyingi liko mwishoni mwa utenzi au zaburi.
Mapokeo hayo yanatokana na desturi za masinagogi ya Wayahudi.[2]
Kati ya Wakristo kwa kawaida doksolojia inaulenga Utatu Mtakatifu, yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Doksolojia zinapatikana katika sala za Ekaristi, Liturujia ya Vipindi, Rozari n.k.
Jina la sala hiyo linatokana na maneno yake ya kwanza. Kwa kirefu ni: Gloria Patri, et Filio, et Spiritui Sancto. Sicut erat in principio, et nunc, et semper, et in sæcula sæculorum. Amen.
Tafsiri yake ni: :Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
Kwa Kigiriki ni: Δόξα Πατρὶ καὶ Υἱῷ καὶ Ἁγίῳ Πνεύματι, καὶ νῦν καὶ ἀεὶ καὶ εἰς τοὺς αἰῶνας τῶν αἰώνων. Ἀμήν.
Tanbihi
hariri- ↑ American Heritage Dictionary, Wordnik, s.v. "doxology".
- ↑ Doxology - Catholic Encyclopedia article
Viungo vya nje
hariri- "Doxology" at New Advent
- Glory Be
- The Glory Be and other prayers of the Rosary in many languages
- A website with the Lord's Prayer in multiple languages; some of the languages also have the Glory Be
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Atukuzwe Baba kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |