Open main menu

Godfrey Mwakikagile

Godfrey Mwakikagile (amezaliwa 4 Oktoba 1949 huko Kigoma) ni mwandishi Mtanzania aishiye nchini Marekani. Anajulikana hasa kwa kuandika wasifu ya marehemu Julius Nyerere.

Ameandika zaidi ya vitabu sitini. Vitabu vyake vingi vinatumiwa vyuoni katika nchi mbalimbali duniani. Ameandika vitabu vya siasa, uchumi, historia na masomo mengine kuhusu bara la Afrika na nchi mbalimbali katika bara hilo. Pia ameandika vitabu kuhusu watu weusi wenye asili ya Kiafrika nchini Marekani, Uingereza na visiwa vya Karibeani pamoja na nchi ya Belize, bara la Amerika, ambayo pia ina asili ya watumwa kutoka Afrika.

Kabla ya kwenda Merekani, Godfrey Mwakikagile alikuwa mwandishi wa habari, Daily News, Dar es Salaam, Tanzania. Pia aliwahi kuwa mwandishi wa habari katika Wizara ya Habari na Utangazaji, Dar es Salaam. Mhariri wa Daily News wakati ule, Benjamin Mkapa, ambaye baadaye alichaguliwa kuwa raisi wa Tanzania, alimsaidia kwenda Marekani kusoma. Alipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Wayne State, Detroit, Michigan, nchini Merekani, Godfrey Mwakikagile alichaguliwa kuwa raisi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiafrika katika chuo hicho.

Amewahi kufundisha sehemu mbalimbali nchini Marekani.

Pia amealikuwa na vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani kwenda kuzungumza na wanafunzi na walimu wa vyuo hivyo kuhusu masuala mbalimbali kwa sababu ya vitabu alivyoandika. Vyombo mbambali vya habari, pamoja na BBC, Voice of America (VOA), PBS (Public Broadcasting Service) ya Marekani na vingine navyo vimemwalika kuzungumza naye kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu bara la Afrika pamoja na viongozi wake na sera zao.

Professor Guy Martin, katika kitabu chake, African Political Thought, ameandika kwamba Godfrey Mwakikagile ni miongoni mwa wasomi wa juu kutoka bara la Afrika ambao ni "populist scholars" na "thinkers" pamoja na viongozi kama Kwame Nkrumah, Mwalimu Julius Nyerere, Amilcar Cabral, Cheikh Anta Diop, Steve Biko, na Claude Ake, katika historia ya bara hilo tangu karne nyingi zilizopita.

Godfrey Mwakikagile anaendelea kuandika vitabu. Kitabu chake ambacho kilichapishwa mwaka 2019, siku yake ya kuzaliwa 4 Oktoba, kinaitwa Conquest of the Mind: Imperial subjugation of Africa.

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Godfrey Mwakikagile kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.