Belize ni nchi ya Amerika ya Kati upande wa pwani ya mashariki.

Belize
Bendera ya Belize Nembo ya Belize
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Kilatini: Sub Umbra Floreo
(maana yake: "Kivulini nasitawi")
Wimbo wa taifa: Land of the Free
Wimbo wa kifalme: God Save the Queen
Lokeshen ya Belize
Mji mkuu Belmopan
17°15′ N 88°46′ W
Mji mkubwa nchini Belize City
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali Nchi ya Jumuiya ya Madola
Charles III wa Uingereza
Froyla Tzalam
Johnny Briceño
Uhuru
Tarehe
Kutoka Uingereza
21 Septemba 1981
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
22,966 km² (151st)
0.8
Idadi ya watu
 - Julai 2022 kadirio
 - 2010 sensa
 - Msongamano wa watu
 
441,471 (ya 168)
324,528
17.79/km² (ya 169)
Fedha Belize Dollar (BZD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-6)
(UTC)
Intaneti TLD .bz
Kodi ya simu +501

-


Inapakana na nchi za Mexiko, Guatemala na Honduras.

Makao makuu yako Belmopan, lakini mji mkubwa zaidi ni Belize.

Historia

hariri

Hadi mwaka 1973 ilijulikana kama koloni la British Honduras (Honduras ya Kiingereza).

Tangu mwaka 1964 koloni lilikuwa na serikali yake na madaraka ya kujitawala katika mambo ya ndani.

Uhuru kamili ukafuata tarehe 21 Septemba 1981.

Uhusiano na nchi jirani ya Guatemala ulikuwa mgumu kwa miaka mingi kwa sababu serikali ya Guatemala ilidai kuwa Belize ni sehemu yake.

Ingawa wakazi si wengi, wana asili tofauti sana. Walio wengi ni machotara: kati yao, 52.9% wana damu ya Waindio zaidi, 32% damu ya Kiafrika zaidi. Wanafuata kwa wingi Waindio asili, Wahindi, Wazungu, Wachina n.k.

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini kwa kawaida zinazungumzwa Krioli (62.6%) na Kihispania (30%).

Upande wa dini, 73.8% ni Wakristo (40.1% ni Wakatoliki na 31.8% Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali). 15.5% hawana dini yoyote.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Belize kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.