Hadja Idrissa Bah

Hadja Idrissa Bah (pia: Hadja Idy; alizaliwa 23 Agosti 1999) ni mwanaharakati wa kike wa haki za watoto kutoka Guinea, ambaye alichaguliwa kuwa rais wa bunge la watoto wa Guinea mwaka 2016. Pia alikuwa mshauri wa Rais Emmanuel Macron kwenye masuala ya wanawake.

Hadja Idrissa Bah

Maisha Edit

Wazazi wake walifanya kazi ya kuuza duka na kufanya usafi, walimsaidia kutimiza ndoto zake za kuhitimu masomo ya sekondari katika shule ya Saint Georges High School huko Conakry.[1] Alisomea sayansi ya siasa kwa mwaka mmoja katika chuo cha University of General Lansana Conté (fr:Université Général Lansana Conté|fr), kabla ya kudahiliwa kwenye kitivo cha sheria katika chuo Sorbonne University (Paris).

Uanaharakati Edit

Mwaka 2016 Bah alichaguliwa kuwa Rais wa bunge la watoto wa Guinea. Kama Rais, aliwataka viongozi wa Guinea kuheshimu haki za watoto: "Haki za mtoto wa Guinea zipo hatika hali ya kutisha, kwa sababu wanasahauliwa."[2] Anajihusisha haswa na vita dhidi ya ukeketaji wa wanawake, cha kukatisha tamaa juu jambo hili ni kwamba "imani potofu zina uzito zaidi ya sheria".[3] Katika kipindi chake cha urais aliongelea waziwazi mambo mbalimbali, ikiwemo: kupinga ndoa za utotoni (teen marriage);[4] sexual and (domestic violence);[3] ubakaji;[5] unyanyapaa wa kijinsia dhidi ya wanawake.[6] Bah alichaguliwa kwenye bunge akiwa na miaka 13.[7]

Mwaka 2016 alianzisha (Guinea Girl Leaders Club), ambayo ilitambua manyanyaso wanayokutana nayo mabinti na wasichana wadogo katika jamii ya watu wa Guinea.[3] Taasisi ilijikita kuwaelimisha wasichana wadogo ambao wanarubuniwa kufunga ndoa katika umri mdogo ili kufikiria mara mbili kabla ya kukubali.[8] Kundi lake lilipingana na wazazi wanaowashawishi mabinti zao kuolewa katika umri mdogo.[9] Pia walianzisha kampeni dhidi ya ukeketaji female genital mutilation, kwa kuzingatia zaidi nyakati za likizo za shule kwenye msimu wa joto - muda ambao mabinti wengi wanakeketwa.[10]

Marejeo Edit

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hadja Idrissa Bah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.