Hali Halisi ni dokumentari kuhusu muziki wa rap nchini Tanzania. Hali halisi (msemo wa kiswahili wenye maana ya "the real situation" kwa kiingereza) inaonyesha rap kama chombo mbadala kwa wasanii kueneza ufahamu juu ya maswala mbalimbali yanayohusu jamii zao. Rapa na wataalamu mbalimbali wanatoa maoni yao kuhusu matukio ya kuibuka kwa miondoko ya hip hop jijini Dar es Salaam na kisiwa cha Zanzibar. Na pia, mawazo yao kuhusu umuhimu wa kurap kama chombo cha mawasiliano.[1]

Hali Halisi - Rap as an alternative medium in Tanzania
Imeongozwa na Martin Meulenberg
Imetayarishwa na Thomas Gesthuizen
Sinematografi Joost Kahmann
Imehaririwa na Patrick Pauwe
Imesambazwa na Madunia Foundation
Imetolewa tar. 1999
Ina muda wa dk. 30
Nchi Tanzania
Lugha

Filamu hii ya dakika thelathini ilirekodiwa mwaka 1999 na Madunia Foundation (wakati huo, shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu nchini Uholanzi ambalo linaunga mkono sanaa ya wanamuzi wa Kiafrika).[2]

Hali Halisi iliongozwa na Martin Maulenberg (alikuwa mwalimu wa shule ya uandishi wa habari huko Utrecht, Uholanzi na utafiti ulifanywa na Thomas Gesthuizen (anafahamika zaidi kwa jina la DJ Jumanne au J4) ni mwanzilishi wa tovuti ya Africanhiphop. com.

Hali Halisi ilishirikisha wasanii maarufu wa hip hop nchini Tanzania kwa wakati huo. Wasanii kama Gangstas With Matatizo ("matatizo") au GWM, Mr II ( 2Proud au Sugu), Deplowmatz, Gangwe Mobb, X Plastaz na Bantu Pound ni miongoni mwa vikundi vya kwanza vya rap nchini Tanzania kupata usikivu wa kitaifa.[3]

Washiriki hariri

Baadhi ya wasanii walioshiriki Hali Halisi:


Wataalam kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na Redio Tanzania pia walishiriki.

Mapokezi hariri

Hali Halisi ilionyeshwa kwenye Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) mwaka 2001 na Vancouver International Hip Hop Film Festival mwaka 2004. Pia imewahi kuonyeshwa na ITV Tanzania na kwenye matamasha mengine ya filamu dunia kote.[4]

Tuzo za H2O hariri

Hali Halisi ilishinda tuzo ya "Best Short Documentary" kwenye toleo la nne la tamasha la filamu la H2O (Hip Hop Odyssey) lililofanyika Novemba 2004 katika ukumbi wa Symphony Space jijini New York, Marekani.[5]

Ilikuwa mara ya kwanza kwa filamu inayohusu utamaduni wa hip hop Afrika Mashariki kukubalika kwa kiwango kikubwa nje ya bara la Afrika.

Tarehe 7 Novemba wakati wa sherehe za tuzo hizo, mwanamuziki Jean Grae alikabidhi tuzo hiyo kwa mtayarishaji mwenza Thomas Gesthuizen. Wasanii waliohudhuria ni pamoja na Afrika Bambaata, DJ Kool Herc, Grandmaster Caz wa kundi la Cold Crush Brothers, kundi la UTFO, Mc Lyte, Dres kutoka kundi la Black Sheep na Lord Jamar kutoka kundi la Brand Nubian. Wasanii wadogo kwa wakati huo kama Jojo (K-Ci na Jojo), Murs na Keith Murray pia walihudhuria.

Mtanzania Dola Soul, ambaye pia alishiriki kwenye Hali Halisi ni moja ya watu waliohudhuria tuzo hizo. Katika tukio hilo tuzo za heshima zilitolewa kwa Kurtis Blow, Queen Latifah, RZA na Russell Simmons. Mtayarishaji mkongwe wa filamu Melvin Van Peebles na mwanamuziki Roxanne Shante walitoa pongezi kwa Madunia Foundation.

Marejeo hariri

  1. "Hali Halisi, rap as an alternative medium in Tanzania". Africanhiphop (kwa en-US). 2009-06-14. Iliwekwa mnamo 2022-06-04. 
  2. Msia Kibona Clark (2006-07-03). "Tanzania: Hali Halisi: Rap as an Alternative Medium in Tanzania". allAfrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-03. 
  3. Msia Kibona Clark (2006-07-03). "Tanzania: Hali Halisi: Rap as an Alternative Medium in Tanzania". allAfrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-04. 
  4. "Hali Halisi [Film]". The Communication Initiative Network (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-03. 
  5. "Hali Halisi, rap as an alternative medium in Tanzania". Africanhiphop (kwa en-US). 2009-06-14. Iliwekwa mnamo 2022-06-03.