Joseph Mbilinyi

Mwanasiasa wa Tanzania, mwanaharakati wa haki za binadamu na mwimbaji wa rap.

Joseph Osmund Mbilinyi (anajulikana sana kwa jina lake la kisanii kama Mr. II na Sugu au 2-proud; amezaliwa 1 Mei 1972) ni rapa, mwanaharakati wa haki za binadamu na mwanasiasa kutoka nchini Tanzania.

Ni miongoni mwa waanzilishi wa awali kabisa wa hip hop ya Tanzania, kwanza akiwa na Da Young Mob, ambao alishirikiana nao katika kinyang'anyiro cha Yo Rap Bonanza iliyokuwa inaandaliwa na akina Kim the Boyz na Ibony Moalim katika miaka ya 1990, kabla ya kwenda kuwa rapa wa kujitegemea na kutoa albamu ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Ni Mimi mnamo mwaka wa 1995.

Vivile Sugu ni mwanasiasa wa Chama cha kisiasa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Mbeya Mjini kwa miaka 20152020.[1][2] [3]

Mwishoni mwa mwezi Agosti, 2017, Sugu alifungua hoteli jijini Mbeya na kuipa jina la "Desderia Hotel".[4]

Diskografia

hariri

Mr. II ndiyo msanii pekee wa hip hop ya Tanzania ambaye katoa albamu nyingi:

Marejeo

hariri
  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
  2. "Microsoft Word – Stichproben_Nr5_FERTIG.doc" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2005-01-10. Iliwekwa mnamo 2017-10-04.
  3. "Bongoflava: The Primer – Pop Playground – Stylus Magazine". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-01-08. Iliwekwa mnamo 2017-10-04.
  4. SUGU AFUNGUA HOTELI YA KIFAHARI Ilihifadhiwa 20 Julai 2018 kwenye Wayback Machine. ingizo la tarehe 1 Septemba, 2017 - wavuti ya Richard Mwambe
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joseph Mbilinyi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.