Magamaga

(Elekezwa kutoka Heliolais)
Magamaga
Magamaga mbavu-kahawia
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Cisticolidae (Ndege walio na mnasaba na videnenda)
Ngazi za chini

Jenasi 8 za magamaga:

Magamaga ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wanafanana na videnenda lakini mkia wao ni mrefu zaidi na hawana michirizi mizito. Spishi za Micromacronus na karibu na nusu ya spishi za Prinia hutokea Asia lakini spishi zote nyingine za magamaga hutokea Afrika. Hawa ni ndege wa maeneo wazi yenye nyasi ndefu na vichaka. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe ndani ya nyasi au kichaka karibu na ardhi; mara nyingi tago limefunika. Jike huyataga mayai 2-5.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri