Hemikodata
Hemikodata | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mnyoo-mkonga (Glossobalanus sp.)
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Ngeli 3:
|
Hemikodata ni faila ya wanyama wa bahari katika faila ya juu Deuterostomia. Wanachukuliwa kama kikundi cha dada cha wanyama ngozi-miiba. Wanatokea kwa mara ya kwanza katika Cambrian ya Chini au ya Kati na wana ngeli kuu mbili: Enteropneusta (minyoo-mkonga) na Pterobranchia. Ngeli ya tatu, Planctosphaeroidea, inajulikana tu kutoka kwa lava wa spishi moja, Planctosphaera pelagica. Ngeli Graptolithina, iliyokwisha sasa, inahusiana sana na Pterobranchia.
Hemikodata ni kati ya jamaa wa karibu zaidi wa kijeni wa Kodata kati ya invertebrata. Kwa hivyo minyoo hao wa bahari ni ya kuvutia sana kwa utafiti wa asili ya maendeleo ya kodata.
Minyoo-mkonga huishi peke yao katika vishimo kwenye sakafu ya bahari (mirija ya kwanza ya kabla ya historia iliyotolewa) na hujilisha kwa mashapo. Lakini spishi kadhaa hutumia nyufa katika koromeo ili kuchuja chembe za chakula kutoka maji. Spishi za familia Torquaratoridae huishi huru na kujilisha kwa maada ogania kwenye sakafu. Pterobranchia huchuja chakula na minyiri yao. Huishi katika makoloni, muundo wa kolajeni kwa umbo la mrija unaoitwa coenecium.
Maelezo
haririMwili wa minyoo-mkonga umegawanyika katika mkonga wa mbele, ukosi wa kati na fumbatio ya nyuma. Mkonga ni ogani yenye misuli na silio (nywele ndogo sana) kwenye ngozi unaotumika kwa kuogelea na kukusanya na kupeleka chembe za chakula. Kinywa kipo kati ya mkonga na ukosi. Fumbatio ni sehemu ndefu zaidi ya mnyama. Ina koromeo iliyotobolewa na nyufa, umio, matumbo marefu na mkundu kwa nyuma kabisa. Gonadi (tezi za kijinsia) zimo ndani ya fumbatio pia.
Sehemu ya mbele ya mwili wa Pterobranchia imetoholewa katika ngao ya kichwa yenye misuli na silio. Hutumika kwa kuogelea na kutoa coenecium. Sehemu ya kati ina jozi moja au mbili za minyiri inayotumika kwa kuchuja chakula kutoka maji. Fumbatio ina matumbo kwa umbo la kitanzi na gonadi ndani yake na inaendelea katika kikonyo kinachoweza kufupishwa na kuunganisha wanakoloni ambao hujalishwa kwa kuchipua bila ngono.
Picha
hariri-
Enteropneusta (Saccoglossus sp.)
-
Pterobranchia (Cephalodiscus dodecalophus)