Herbert Grönemeyer
Herbert Arthur Wiglev Clamor Grönemeyer (amezaliwa tar. 12 Aprili 1956) ni mwigizaji na mwanamuziki maarufu kutoka nchini Ujerumani. Anafahamika sana kwa nchi ya Ujerumani, Austria na Switzerland. Amecheza kama mwandishi wa habari wa vita Lieutenant Werner kwenye filamu ya Wolfgang Petersen Das Boot, lakini baadaye akazingatia zaidi shughuli zake za kimuziki. Albamu yake ya tano inaitwa 4630 Bochum (1984) na albamu yake ya ishirini inaitwa Mensch (Binadamu) (2002) ni rekodi za lugha ya Kijerumani zilizouza vizuri kwa muda wote.
Herbert Grönemeyer | |
---|---|
Herbert Grönemeyer, 2004
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Herbert Arthur Wiglev Clamor Grönemeyer |
Amezaliwa | 12 Aprili 1956 |
Asili yake | Göttingen, Lower Saxony, Ujerumani |
Aina ya muziki | Rock, Pop, Soft rock |
Kazi yake | Mwimbaji, Mwigizaji, Mtunzi |
Miaka ya kazi | 1978–1988, 1990–mpaka sasa |
Studio | EMI, Co.KG |
Ame/Wameshirikiana na | Pop 2000 |
Tovuti | http://www.groenemeyer.de/ |
Maisha ya awali
haririGrönemeyer mara nyingi huelezea asili ya maisha yake binfasi kwamba yamelala katika mji wa Kijerumani wa Bochum ambapo ametumia maisha yake ya utotoni kwa kiasi kikubwa, ujana na utu uzima wa awali. Hadi leo, wimbo wa Bochum, aliutoa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984, ni moja kati ya nyimbo za alama yake, hasa wakati anatumbuiza kwenye makumbi. Kuzaliwa kwake mjini Göttingen na sio mjini Bochum ana maelezo yake mwenyewe: "Nimezaliwa mjini Göttingen tu kwa sababu mama yangu alikuwa akizimia mara kwa mara wakati ana ujauzito wangu. Amefanya hivi kila mara amejigeuza upande wake wa kushoto, na hakuna hata mmoja aliyemwamini. Mjini Göttingen kulikwa na profesa, mtaalamu, naye hakumwamini vilevile, kwa kilele hicho kalala chini, kazimia, na kuniletea mimi kwenye ulimwengu huu. Hii ndiyo sababu nimezaliza mjini Göttingen."
Kazi
haririDiskografia
haririAlbamu
hariri- 1978 — Ocean Orchestra
- 1979 — Grönemeyer
- 1980 — Zwo
- 1982 — Total egal
- 1983 — Gemischte Gefühle
- 1984 — Bochum
- 1986 — Sprünge
- 1988 — Ö
- 1988 — What's all this
- 1990 — Luxus
- 1991 — Luxus (English)
- 1992 — So gut
- 1993 — Chaos
- 1994 — Cosmic Chaos
- 1995 — Unplugged
- 1995 — Live
- 1996 — Chaos (English)
- 1998 — Bleibt alles anders
- 2000 — Stand der Dinge (Double DVD/CD)
- 2002 — Mensch
- 2003 — Mensch live (Double DVD)
- 2006 — "Zeit, dass sich was dreht" / "Celebrate the day" (Official 2006 FIFA World Cup Anthem) (Maxi CD)
- 2007 — 12
- 2008 — Was muss muss
Filmografia
hariri- 1976 — Die Geisel (imeongozwa na Peter Zadek)
- 1978 — Von Tag zu Tag (imeongozwa Ulrich Stein)
- 1978 — Uns reicht das nicht (imeongozwa na Juergen Flimm)
- 1979 — Daheim unter Fremden (imeongozwa na Peter Keglevic)
- 1981 — Das Boot (imeongozwa na Wolfgang Petersen)
- 1982 — Doktor Faustus (imeongozwa na Franz Seitz)
- 1982 — Frühlingssinfonie (imeongozwa na Peter Schamoni)
- 1984 — Die ewigen Gefühle (imeongozwa na Peter Beauvais)
- 1985 — Väter und Söhne (imeongozwa na Bernhard Sinkel)
- 2007 — Control (imeongozwa Anton Corbijn)
- 2010 — The American (imeongozwa na Anton Corbijn)
Viungo vya Nje
hariri- http://www.groenemeyer.de Official site
- http://www.groenland.com Grönemeyer's record label
- http://www.letzte-version.de Ilihifadhiwa 7 Juni 2023 kwenye Wayback Machine. Fan site
- Herbert Grönemeyer on Europopmusic.eu Ilihifadhiwa 21 Desemba 2010 kwenye Wayback Machine. (English)
- Herbert Grönemeyer kwenye Internet Movie Database