Hermoni
33°24′58″N 35°51′27″E / 33.41611°N 35.85750°E
Hermoni (kwa Kiarabu: جبل الشيخ, jabal-ash-Shaikh, yaani "mlima wa shehe"; kwa Kiebrania: הר חרמון, Har Hermon) ni mlima wa Siria na Lebanoni ulio mrefu kuliko yote ya safu ya Lebanoni Ndogo na ya Siria nzima, ukiwa na kimo cha m 2,814 juu ya UB.
Kileleni kuna theluji ya kudumu na ni chanzo cha mto Yordani.
Unatajwa katika Biblia (Zaburi 42; 133:3; Wimbo Ulio Bora 4:8).