Wimbo Ulio Bora
Wimbo Ulio Bora (kwa Kiebrania שיר השירים, Shir ha-Shirim), ni kitabu kimojawapo cha Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia cha Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Utunzi wake
haririIngawa mapokeo yanamtaja mfalme Solomoni kama mtunzi, wataalamu wanaona ni kazi ya mwandishi wa karne ya 4 KK aliyekusanya nyimbo mbalimbali za mapenzi.
Aina ya uandishi
haririNi kati ya vitabu vya kishairi na vya pekee zaidi katika Biblia, kwa kuwa kinaimba mahaba ya wapenzi wawili, ambao wanatafsiriwa kama wawakilishi wa Mwenyezi Mungu na taifa lake, kadiri ya moja kati ya mafundisho makuu ya ufunuo, linalotokana na nabii Hosea.
Ndio ujumbe wa kitabu: upendo kati ya mume na mke unaweza na kutakiwa kufanana na ule kati ya Yesu Kristo na Kanisa lake.
Maneno ya bibiarusi (Wim 8:6-7)
hariri"Nitie kama muhuri moyoni mwako,
kama muhuri juu ya mkono wako;
kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
Mwako wake ni mwako wa moto,
na miali yake ni miali ya Bwana.
Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,
wala mito haiwezi kuuzamisha.
Kama mtu angetoa badala ya upendo mali yote ya nyumbani mwake,
angedharauliwa kabisa".
Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki
Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wimbo Ulio Bora kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |