Hifadhi ya Mkomazi

Hifadhi ya Mkomazi ipo katika mikoa miwili ambayo ni Kilimanjaro na Tanga, ndani ya wilaya za Same na Lushoto nchini Tanzania.

Kifaru Mweusi.
Kifaru Mweusi.

Hifadhi ya Mkomazi ilianzishwa mnamo mwaka 1951 kama Pori la Akiba lililotengwa kutoka katika Pori kubwa la Akiba la Ruvu.

Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 3245 (kilometa za mraba 2010.4 ni Mkomazi na kilometa za mraba 1224.1 ni Umba).

Pori hili lilipendekezwa kuwa hifadhi ya taifa kwa misingi ya kunusuru maeneo na rasilimali zilizomo kutokana na matumizi yasiyoendana na uhifadhi kwa ajili ya kizazi cha leo na kijacho.

Katika hifadhi hii kuna wanyama na ndege wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbwa pori na vifaru weusi walioingizwa kutoka nchi ya Afrika Kusini.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania

Viungo vya nje hariri