Wilaya ya Same
Wilaya ya Same ni wilaya moja kati ya wilaya 7 za Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 269,807.[1]
WIlaya hii imepakana upande wa kazkazini na Wilaya ya Mwanga na nchi jirani ya Kenya, upande wa kusini na Mkoa wa Tanga na upande wa magharibi na Mkoa wa Manyara. Makao makuu yapo Same Mjini.
Upande wa kusini ya Milima ya Pare upo ndaniy a wilaya pamoja na sehemu ya Hifadhi ya Mkomazi.[2]
Njia ya reli ya Usambara inapita wilayani.
MarejeoEdit
- ↑ Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Same DC[dead link]
- ↑ (June 2015) Tanzania travel guide, 6, Lonely Planet, 148. ISBN 978-1742207797. Retrieved on 12 January 2016.
Viungo vya NjeEdit
- Same Profile, Kilimanjaro Region website Archived 26 Machi 2016 at the Wayback Machine.
Kata za Wilaya ya Same - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bangalala | Bendera | Bombo | Bwambo | Chome | Gavao Sawene | Hedaru | Kalemawe | Kihurio | Kirangare | Kisima | Kisiwani | Lugulu | Mabilioni | Makanya | Maore | Mhezi | Mpinji | Mshewa | Msindo | Mtii | Mwembe | Myamba | Ndungu | Njoro | Ruvu | Same Mjini | Stesheni | Suji | Tae | Vudee | Vuje | Vumari | Vunta|}
|