Hipparchos wa Nikaia

(Elekezwa kutoka Hipparchus)

'

Hipparchos wa Nikaia
Kazi yakemtaalamu wa astronomia


Hipparchos (kwa Kigiriki Ἵππαρχος; takr. 190 KK hadi takr. 120 KK) alikuwa mtaalamu wa astronomia, jiografia na hisabati wa Ugiriki ya Kale.

Alizaliwa mjini Nikaia (leo: Iznik katika Uturuki) akafariki kwenye kisiwa cha Rhodos.

Hutazamwa kama mwanaastronomia muhimu kabisa wa nyakati za kale.

Aliorodhesha nyota 800 na kuzichora katika ramani ya anga. Alibuni mfumo wa kutofautisha nyota kwa mwangaza unaoonekana. Anaaminiwa ni yeye aliyetunga orodha ya nyota iliyotumiwa miaka 300 baadaye na Klaudio Ptolemaio na kuingizwa katika kitabu chake cha Almagesti kilichoendelea kuwa kitabu kikuu cha astronomia kwa Waislamu na Wakristo wa Ulaya kwa miaka 1500 iliyofuata.[1]

Kwa kutumia paralaksi alipima umbali baina ya Dunia na Mwezi akifaulu kufikia namba iliyo karibu sana na kipimo cha kisasa cha kilomita 384,400 kwa wastani. [2]

Aliweza kukadiria na kutabiri kupatwa kwa jua .

Katika hisabati alianzisha mbinu za kijiometria, kwa mfano mgawanyo wa duara kuwa na nyuzi 360.

Marejeo

  1. Pickering, The Southern Limits of the Ancient Star Catalog and the Commentary of Hipparchos, The International Journal of Scientific History, Vol. 12 2002 Sept ISSN 1041›5440,
  2. G. J. Toomer, "Hipparchus on the distances of the sun and moon," Archive for History of Exact Sciences 14 (1974), 126–142