Rhodos katika Ugiriki

Rhodos ni kisiwa cha Ugiriki karibu na pwani la Uturuki.

Kuna takariban wakazi 120,000. Miji mikubwa ni Rhodos na Lindos.

Rhodos ina historia ndefu.

Katika nyakati za kale ilikuwa na Sanamu ya Kolossos iliyohesabiwa kati ya maajabu ya dunia.

Wakati wa vita za misalaba kisiwa kilikuwa kituo muhimu ya wamisalaba wa chama cha hospitali ya Mt. Yohane wa Yerusalemu. 1644 Waosmani walifaulu kuteka kisiwa na wamisalaba walihamia Malta.

Mwaka 1912 kisiwa kikatwaliwa na Italia na kuwa sehemu ya Ugiriki ya kisasa tangu 1946.

Uchumi wa kisiwa hutegemea hasa utalii.