Hiroglifi
Hiroglifi (Kigiriki: ἱερογλύφος iero-glifos alama takatifu) ni mwandiko unaotumia picha kwa maneno na silabi, hasa wa Misri ya Kale. Jina "alama takatifu" lilitokana na imani ya kwamba mungu aliwapa watu alama hizi kwa sili yao ilikuwa takatifu.
Aina za hiroglifi
haririMwandiko wa hiroglifi ilitumia picha zilizosanifishwa kama alama za maandishi. Wamisri walitumia alama hizi kwa njia tatu:
a) Hiroglifi kadhaa zilimaanisha kitu kilekile kilichoonyeshwa kwa alama au picha yake zikasomwa kwa kama neno la kutaja kile kilichoonyeshwa
b) Hiroglifi mara nyingi zilisomwa kama alama ya sauti. Sauti hii ilitokana na neno la kitu kilichoonyeshwa kwa alama. Kwa mfano neno kwa "mdomo" lilikuwa "re"; alama ya mdomo lilitumiwa kama "r".
c) wakati mwingine alama hazikusomwa bali zikatumiwa kama maelezo ya alama iliyotangulia. Alama kwa "mwanaume" au "mwanamke" ziliongezwa mara nyingi kuonyesha kama mnyama ilikuwa dume au kike.
Walikuwa na njia nyingi kuunganisha alama hizi kwa kutaja maana za undani zaidi.
Hiroglifi zenyewe mara nyingi zilichongwa kwenye jiwe kwa sanamu au ukutani. Zilichorwa pia ukutani na hadi leo mifano mingi imehifadhiwa kwenye kuta za makaburi ambako maandishi ya kale na picha zilihifadhiwa dhidi ya hali ya hewa, upepo, mvua na mishale ya jua.
Historia ya hiroglifi za Misri
haririHiroglifi zilianza kutumiwa nchini Misri wakati wa milenia ya 4 KK. Mifano ya kale imepatikana katika kaburi lililojengwa mnamo mwaka 3,500 KK. Waandishi waliheshimiwa katika jamii maana walikuwa na kipindi kirefu cha masomo na Wamisri wengi hawakujua kuandika wala kusoma.
Mwanzoni maandishi yalikuwa na alama 700 tu lakini katika karne nyingi za maisha ya mwandiko huo idadi ya alama iliongezeka hadi kufikia 7000.
Kwa kusudi la kuandika haraka kwenye karatasi aina za papiri Wamisri walianzisha staili nyingine iliyofupisha na kurahisisha alama hizi zaidi.
Mtindo huu baadaye ulikuwa chanzo cha alfabeti ya Kifinisia na ya Kiebrania.
Tangu kuvamiwa kwa Misri na Waroma hiroglifi zilisahauliwa polepole na kutumiwa na watu wachache tu. Mfano wa mwisho ambako maandishi yaliandikwa kwa kutumia hiroglifi ilikuwa karne ya 4 BK.
Baadaye maana ya alama hizi yalisahauliwa kabisa. Ni katika karne ya 19 ya kwamba mtaalamu Mfaransa Jean-François Champollion na wengine waliweza kugundua upya maana ya mwandio huo baada ya kupatikana kwa jiwe la Rosetta ambako tangazo la farao Ptolemaio V liliandikwa kwa Kigiriki, hiroglifi na Kimisri kwa mwandiko wa mkononi. Kupitia Kigiriki kilichosomeka wataalamu walifaulu kugundua kwanza majina ya wafalme halafu maana ya alma mbalimbali.
Hiroglifi nje ya Misri
haririNeno "hiroglifi" lataja pia mwandiko unaotumia picha zilizosanifishwa kama alama za maandishi kwa jumla. Mtindo huo ulitumiwa katika tamaduni mbaimbali.
Mfano unaojulikana zaidi nje ya Misri ni mwandiko wa Wamaya waliokuwa wenyeji wa Meksiko kusini.
Viungo vya Nje
hariri- Ancient Egyptian Hieroglyphics - Aldokkan
- Glyphs and Grammars Resources for those interested in learning hieroglyphs, compiled by Aayko Eyma.
- Hieroglyphics! Archived 2012-12-05 at Archive.today Annotated directory of popular and scholarly resources.
- Egyptian Hieroglyphic Dictionary Ilihifadhiwa 1 Novemba 2011 kwenye Wayback Machine. by Jim Loy
- Hieroglyphic fonts Ilihifadhiwa 3 Agosti 2010 kwenye Wayback Machine. by P22 type foundry
- GreatScott.com's Hieroglyphs Ilihifadhiwa 25 Januari 2007 kwenye Wayback Machine. Commercial (free intro)
- Wikimedia's hieroglyph writing codes
- Ancient Egypt Online: Sign list, tutorials and quizzes A complete sign list, plus tutorials and quizzes
- Unicode Fonts for Ancient Scripts Ilihifadhiwa 21 Julai 2011 kwenye Wayback Machine. Ancient scripts free software fonts
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hiroglifi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Egyptian hieroglyphs]]